Ulivyotoka mkoani ulifanikiwa kupanda mwendokasi?

Ulivyotoka mkoani ulifanikiwa kupanda mwendokasi?

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Hapa nazungumzia watu waliofika Dar mara moja na kuondoka siyo kukaa. Exprience yako ya mwendokasi iko namna gani?

Mwendokasi ni mradi unaoiweka sana Dar kwenye ramani. Si ndani ya Tanzania tu, hata huko duniani watu wanausifia sana sana.

Mimi kama mwaka 2020 nilifika Dar na kusema ngoja nikapande Mwendokasi nione uko vipi. Nikakata tiketi. Ndani nikakuta abiria kibao wanasubiria mabasi. Kama mawili yalipita bila kusimama nikiwa pale. Tukasubiri kwa muda mrefu ndiyo likapita lingine na kusimama. Limejaa hadi mlangoni.

Nikaona mtu mmoja wa makamo, kachomekea vizuri akijibanzabanza hadi akaingia. Kwa muda niliosimama pale na hali niliyoiona ya jinsi watu wanavyoingia nikahairisha huko kuexperience Mwendokasi kwenyewe. Ikabidi nisamehe pesa yangu nikapande daladala. Kwa kweli ule siyo usafiri wa kumfaa binadamu kabisa.

Vipi wewe experience yako na mwendokasi, maana najua wengi huwa tunatamani kuujaribu usafiri huu unaosifika Afrika kote.
 
Umepanda mwendokasi 2020, alaf ushuhuda na maswali umekuja kuandika leo mkuu, au kuna kitu umelenga ambacho kimetokea leo?
 
OIG (19).jpeg
 
Back
Top Bottom