Uliwezaje kumudu maisha ya vijijini baada ya kuhamia /kuajiriwa huko?

Uliwezaje kumudu maisha ya vijijini baada ya kuhamia /kuajiriwa huko?

Riskytaker

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2024
Posts
568
Reaction score
2,522
Maisha ya vijijini yanashangaza sana unaweza kujiuliza hawa watu huwa hawapati pesa au shida nini.

Msosi shida, usafiri shida, nyumba shida, maji shida, yaani kila kitu shida. Hii imepelekea what we call suffering ndo imekuwa furaha ya wakazi wengi wa vijijini.

Watu wanaishi tu ili mradi siku ziende hey, wakazi wa vijijini amken mken kumekucha.
 
Yaani vijijini hawajali sijui kuoga kupendeza ....kupaka mafuta yaani wanalalla hivyo hivyo wakiamka safari muziki.....hakuna hata mpangilio wa maisha....watoto wanajilea wenyewe kupika ni majaliwa baadhi ya kaya
 
Kijijini watu wana maisha yenye furaha kuliko huko mjini.
Kuna mchina aliwahi kusema, watz tuna maisha magumu ila anashangaa tunaonekana hatujui kama tuna masiha amgumu na tunafuraha. Mtu akizaliwa na kukulia mazingira fulani, anaona ni kawaida kwa sababu huwezi kumiss au kusumbuliwa na kutokuwepo kwa kitu ambacho hujawahi kuwa nacho.
Zamani kabla ya simu ilikuwa maisha fresh, unaandika barua unasubiri kujibiwa. Sasa hivi kwa sababu tuna simu ni kama maisha hayawezi kuendelea bila simu.
 
Yaani vijijini hawajali sijui kuoga kupendeza ....kupaka mafuta yaani wanalalla hivyo hivyo wakiamka safari muziki.....hakuna hata mpangilio wa maisha....watoto wanajilea wenyewe kupika ni majaliwa baadhi ya kaya
🤣🤣 Mtu analala miguu imetoka shamba afu fresh tu
 
Mikoani kuna dhiki sana. Ndio maana wengi wakifika mijini hawataki kujitambulisha wametokea wapi!
 
Ajira yangu ya kwanza ilikua kijijini, bush kabisa......niseme tu maisha ya kule watu wanafuraha sana, hawana hizi stress za huku mujini, nlikua hata sina cha kutumia pesa zangu, nakaa tu na hela ndani, wanakijiji wana upendo mnooo nlikua napewa vyakula twaishi vizuri, ikifika weekend kulikua na mtumishi mwenzangu mzee anakaribia kustaafu, ananiijia "babuu vipi unalala sahivi twende mnadani" ananipakia kwenye baiskeli tunaenda kula nyama na bia.....ilikua raha sana.
 
Maisha ya vijijini yanashangaza sana unaweza kujiuliza hawa watu huwa hawapati pesa au shida nini.

Msosi shida, usafiri shida, nyumba shida, maji shida, yaani kila kitu shida. Hii imepelekea what we call suffering ndo imekuwa furaha ya wakazi wengi wa vijijini.

Watu wanaishi tu ili mradi siku ziende hey, wakazi wa vijijini amken mken kumekucha.
Njooni huku tulime acheni kujaza mjini huko na kazi hamna mnaishia kuuza madako.
 
Ni experience ngumu kidogo kuvumilika...

Nilikuwa Kila baada ya wiki mbili natoroka Kurudi DSM as ilikuwa ni mwendo wa masaa 8 hivi kufika DSM
 
Usipokua makini na ukajifanya kuzoea maisha ya kijijini unakua mjinga hakuna la maana utafanya
 
Maisha ya vijijini yanashangaza sana unaweza kujiuliza hawa watu huwa hawapati pesa au shida nini.

Msosi shida, usafiri shida, nyumba shida, maji shida, yaani kila kitu shida. Hii imepelekea what we call suffering ndo imekuwa furaha ya wakazi wengi wa vijijini.

Watu wanaishi tu ili mradi siku ziende hey, wakazi wa vijijini amken mken kumekucha.
Shida ipo kwako wewe ambaye umewaza hivyo lakini watu wengi hawawazi sababu hawana mtu wa kuwavusha bahari ya shamu wakati ww ndo umekimbilia mjini Sasa kijiji Kitatendelea vipi !🫡😂🤣
 
Back
Top Bottom