Uliyeiba dera la dada huyu lirudishe kabla hayajakukuta makubwa

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Muda mchache uliopita nikiwa nimetulia zangu mahali nikasikia dada mmoja analalamika kuwa dera lake ambalo alilinunua kwa mkopo wiki chache zilizopita limeibwa wakati alipokuwa amelianika. Na zaidi dada huyo alikuwa analalamika kuwa hata mkopo wenyewe hajamaliza kulipa lakini tayari dera limeibwa.

Kwa hiyo kutokana na maumivu hayo nikamsikia akisema kuwa simu yake ikishajaa chaji tu, atampigia mtaalamu, ili mtendee manuva huyo mwizi wa dera lake. Kwa hiyo kwa kuwa mimi sipendi mtu apigwe kasumba kisa tu dera nimeamua kutoa taarifa kwa uma kuwa kama unajijua leo umeanua dera ambalo sio lako iwe kwa makusudi au bahati mbaya, lirudishe kwa mwenyewe kabla simu yake haijajaa chaji.

Ukichelewa simu ikapigwa kwa mtaalamu, my dear sister/brother, umekwisha. Dera litakutoa roho, Usijesema sikukuambia
 
Huyo sister bado yuko around hapo ulipo?

Nataka kuunganisha order hapo na simu yangu waliyoipitia wahuni ka' vipi chonga naye amu-alert babu yake kabisa

Maana juzi nilipita chocho siyo nikahisi ni njia kumbe ni camp la wahuni wananyonga ganja

Sina mengi ni hayo tu
 
Muda mchache uliopita nikiwa nimetulia zangu mahali nikasikia dada mmoja analalamika kuwa dera lake ambalo alilinunua kwa mkopo wiki chache zilizopita limeibwa wakati alipokuwa amelianika. Na zaidi dada huyo alikuwa analalamika kuwa hata mkopo wenyewe hajamaliza kulipa lakini tayari dera limeibwa.

Kwa hiyo kutokana na maumivu hayo nikamsikia akisema kuwa simu yake ikishajaa chaji tu, atampigia mtaalamu, ili mtendee manuva huyo mwizi wa dera lake. Kwa hiyo kwa kuwa mimi sipendi mtu apigwe kasumba kisa tu dera nimeamua kutoa taarifa kwa uma kuwa kama unajijua leo umeanua dera ambalo sio lako iwe kwa makusudi au bahati mbaya, lirudishe kwa mwenyewe kabla simu yake haijajaa chaji.

Ukichelewa simu ikapigwa kwa mtaalamu, my dear sister/brother, umekwisha. Dera litakutoa roho, Usijesema sikukuambia
Unadhani aliyeiba hilo dela anaweza akawa yuko humu JF. Ili kumsaidia ni vyema ukaenda kupiga mbiu kwenye eneo la tukio.
 
Mtoa mada nadhani ungetuma kwenye grupu la whatsapp la mtaani kwenu huku wengine tunaishi New York haya mambo unayoongea hata hatukuelewi.

Halafu hama huku madongo kuinama otherwise JF sio hadhi yako
 
Madongo kuinama sihami na jf sihami.
 
Pamoja na gharama ya mtaalamu kuwa kubwa, atamkomesha kwa faida ya wengi
 
Mwambie baadae nitailudia na ile chupi nyekundu aliyo anika mwisho wa kamba.
 
Back
Top Bottom