JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Aliyeugua na kupona ana nafasi nzuri zaidi ya kuwaelimisha wengine juu ya dalili za ugonjwa na namna ya kujikinga na kupata nafuu haraka
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika, kuna uwezekano wa kuambukizwa COVID19 zaidi ya mara moja hivyo taratibu za kawaida za kujikinga ni muhimu
1. Kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka au kutumia kitakasa mikono
2. Kuepuka kushikana mikono au kugusana/kukumbatiana na watu
3. Kuepuka mikusanyiko na kutoka nyumbani pale inapokuwa na umuhimu sana huku ukiwa umevaa Barakoa
4. Kuongeza umakini na kuzingatia taratibu unapoenda sehemu za umma kama sehemu za starehe, saluni, benki na matamasha mbalimbali
Upvote
0