Hujatoa juu ya njia sahihi ya kunenepesha Mbuzi, aina ya vyakula na uwalishaje na nikwamuda gani, ili wafikie kilo ngapi kwa Mbuzi jike ua Dume
✓Njia sahihi ya kunenepesha mbuzi.
Kwanza,kabisa njia sahihi ya kunenepesha mbuzi ni kwakutumia mfumo wa zero grazing(yaani kuwalishia kwa ndani) au kwakutumia hay(malisho ya majani ya kukauka) ambayo utunzwa kwa mda katika mifuko midogomidogo mithili ya mikate.
pili,ni kwakuwapatia chanjo ya CCCP walau Mara 1 Kika mwezi kwa miezi miitatu kwa mbuzi mtoto na Mara Mara moja kwa miezi mitatu baada ya kuachishwa kunyonya.
Kutokupigwa ili kumuepusha na stress maana upelekea kutokula vizuri na kupungua uzito.
Kutengenezewa mabanda yasiyona uwezo wakupitisha mvua/miale ya jua.
Banda kuwa mbali na vyanzo vya maji hasa yaliyo tuama.
Banda kuwa na sehemu ya kutokea taka na maji pindi litakapo hitajika kusafishwa.
✓Aina ya vyakula kwa sababu ya kunenepesha.
Kwanza,mbuzi wanahitajika kula walau 50% hadi 55% ya majani kuliko Aina yeyote ile.
Pili,20% ya protein
Tatu,20%concetrates
Nne, 5% Vitamin
Tano,5% madini
✓Namna ya kuwalishia mbuzi wa kunenepesha.
Hapa watakishwa kwa njia ya kawaida maana wanakuwa wamefungiwa katika zizi,lakini ukumbuke pia wanaweza kutolewa kwenda kulishwa.
Kama watalishwa wakiwa zizini,maana yake itahitajika mchanganyo maalumu wakulishwa kwa kila mbuzi.
Kitaalamu inashauliwa kila mbuzi alishwe 1/3 ya uzito wake(kwa mfano Kama mbuzi Ana 40kg inatakiwa alishwe 4kg*1/3 ya uzito wake.
✓Mda mahususi wa kulishwa mbuzi wa kunenepeshwa.
Kitaalamu inashauliwa mbuzi wakunenepeshwa alishwe kwa mda wa mwaka 1 hadi 1.5 ili aweze kukupatia faida,maana akizidisha hapo ataanza kupungua na Mwisho wa siku ukimuuza utamuiza kwa hasara maana ataanza kupoteza uzito.
N.B: lengo la kunenepesha mbuzi ni kwa ajili ya biashara ili aweze kutupatia faida na sivinginevyo.
~kigoma.