Uliza chochote usichokijua na anayekijua atakujibu

Nipe tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali?? Je wajasiriamali wote ni wafanyabiashara au wafanyabiashara wote ni wajasiriamali au yote sawa??

Swali lako ni sawa na kuuliza Jambazi na Kibaka wana tofauti gani wakati unajua fika kuwa lengo lao wote ni moja.
 
Vifaa original na spea za simu kwa dar vinapatikana maduka gani?
kwenye kampuni OFFICIAL ya simu mfano simu ya samsung ni mtaa msimbazi mkabala na azam stendi ya zamani ya mbagara jengo linaangaliana na stand ya mabasi ya mwendokasi ya gerezani
agrey yote ni copy ila spea zinapatikana pia na zinafanya kazi vizuri tu
 
wakili msomi maana yake nn? kwanini asiitwe tu wakili
 
Nani anayefanya mauaji huko mkoani Pwani wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga?
Hili swali lako linahitaji upembuzi na uchunguzi wa kina, in fact hongera sana kwa kuwawazia waTanzania wenzako.
Sasa fanya tukutane Dunia Duara ili nione nakujibu kutokea kwenye angle ipi.
 
Ningependa kujua maana halisi ya kufika KILELENI!!!!
Ni wachache walio/wanao fika KILELENI...

Mlima Kilimanjaro kuupanda sio swala la KUKURUPUKA.

Yanatakiwa maandalizi, ki-mwili na ki-akili..

Mtanzania wa kwanza kufika KILELENI tunaambiwa ni yule MWANAJESHI MZALENDO, aliyeupandisha MWENGE wa UHURU..[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Ni kitendo cha kuchukua kiasi kikubwa cha pesa za umma kwa maslahi binafsi.
Mzee huo ni ufisadi, siyo kutakatisha fedha.
Ningependa kufahamu maana ya kutakatisha fedha
Kutakatisha fedha ni kuchukua pesa ambayo chanzo chake ni kichafu kisha kuipitishia katika chanzo halali.

Mfano muuza dawa za kulevya pesa yake ni chafu hivyo anaweza akajenga nyumba na kupangisha kodi atakayolipwa ni pesa safi.
Au akaiingiza katika mzunguko wa biashara halali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…