Hakuna kitu kinachoitwa sponsored page. Ila kuna sponsored post ambayo ni post za Facebook au Instagram zinazolipiwa kwa ajili ya kuendesha matangazo.
Kufanya hivyo fuata hatua zifuatazo:
- Hakikisha una kurasa ya biashara kwenye Facebook (business page). Kwa maelekezo jinsi ya kufanya hivyo, kasome blog post yetu ya 'Jinsi Ya Kuanzisha kurasa Ya Biashara Kwenye Facebook' hapa.
- Weka tangazo lako kwa kufuata linki ifuatayo: Se connecter à Facebook | Facebook
- Chagua aina ya tangazo unalotaka
- Walenge watu husika
- Chagua wapi unataka tangazo lako lionekane. Hakikisha Intagram inakuemo katika chaguo lako.
- Lipia tangazo lako. Kufanya hivyo utahitaji visa/mastercard au paypal.
Japokuwa kuna maelezo ya kina natumai utakuwa umepata mwanga.
Nategemea siku za karibuni kuandika post ya kina ya Jinsi Ya Kuweka matangazo kwenye Facebook na Instagram. Nita share humu ili na wewe upate faida.