Huu ni uzi maalumu kwajili ya kupeana directions mbalimbali za sehemu tunapoenda ili kuepusha usumbufu unaoweza kuepukika au kupelekea mgeni kupotea kabisa.
Naamini JF ina members kutoka pande zote za Tanzania hivyo itakuwa rahisi kupewa ramani na kufika sehemu husika kwa usalama na uhakika zaidi. KARIBUNI.
Nipo Mwanza maeneo ya nyegezi mda huu, ninataka kwenda sehemu moja inaitwa NYANGUGE. kwa wanaokifahamu hicho kijiji, naomba mnielekeze kiko wapi au nipande gari zipi?