Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Daisle Simon Ulomi Kwa Sasa ni marehemu baada ya maiti yake kukutwa Jana hospitali ya rufaa Mwananyamala. Taarifa za Jeshi la Polisi na Msemaji wa hospitali hiyo zinadai alipelekwa hapo jioni ya tarehe 11.12.2024 akiwa tayari amefariki Kwa ajali ya pikipiki MC 415 DQC. Ndugu zake akiwemo mkewe walithibitisha kutoweka Kwa ndugu yao mapema asubuhi 11.12.2024 Kwa madai ya kuitika wito wa TRA àmbao jioni ya 15.12.2024 walikanusha kuwasiliana na Ulomi.
Baada ya tukio Hilo kumekuwa na Taarifa toka vyanzo mbalimbali wakiwemo watu binafsi na hata Askari Polisi kuwa Daisle Simon Ulomi alikuwa ni mwajiriwa wa Jeshi la Polisi Tangu mwaka wa fedha 2005/06. Habari hizi hazijakanishwa na Jeshi la Polisi na hivyo wanaoamini hivyo wanaendelea kueneza Jambo wasilo na uhakika nalo.
Mkanganyiko zaidi unakuja kama kweli ni Polisi au aliwahi kuwa Polisi na tena wasemaji wanadai amefanya kazi traffic Ilala, mbona Taarifa ya Kamanda kanda maalum ambaye ni Wazi huyu ni mwajiriwa wake (Kama kweli ni Polisi) hamsemi lolote juu ya Utumishi wake zaidi ya kumtaja kama Mfanyabiashara ?
Iwapo itakugundulika baadaye kweli Daisle alikuwa Polisi haitasababisha Imani mbaya juu ya utendaji wa Jeshi la Polisi kupata nguvu?
Unaanzaje kumkana mwanao hata kama wanasema wewe ndo umemloga?
Labda iwe uongo akiwemo mke wa marehemu aliyetamka hivyo labda alikuwa hajui kazi halisi ya mumewe maana Vijana mjini Wana Mambo mengi, lakini ikiwa ni kweli Ulomi "aliyefariki Kwa ajali" alikuwa Polisi, Mamlaka zilizo juu ya Polisi zina wajibu wa kufanya kitu juu yao.