Ultimate Guide : Jinsi ya kutengeneza Pesa UpWork mwaka unakuja 2020

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
767
Reaction score
1,657
Greetings JF massive

Imekuwa muda kidogo sijaandika hapa kwasababu ya majukumu lakini leo nimepata time kidogo nikasema nitatumia muda huu ku-share mambo muhimu kabisa katika darasa la leo.

Kwanza kabisa niseme mwaka 2020 utakuwa mwaka wa kazi na pesa. Kama ilivyokuwa mwaka huu unaoisha 2019 basi 2020 itakuwa hivyohivyo kwasababu secret ni ile ile. Kuweka malengo na kuhakikisha nafanya kila kinachowezekan kupata nachotaka.

No fear. Only ambition.

Binafsi nikifanya reflection kwa Hustle zote nilizofanya kama freelancer kwa mwaka huu unaoisha 2019 natabasamu tu nakufurahi.

2019 nimetengeneza good money. Lakini pia nimejenga trust kwa kila client ninayefanya naye kazi.



Note : Nimeficha majina kwa ajili ya privacy ya client wangu.

Ok tuendelee.

Kama nilivyosema darasa la leo ni kufahikisha mwaka 2020 ni kupiga kazi na Kutengeneza pesa.

Hapa nitakuonyesha mbinu nilizotumia binafsi kupata kazi lakini pia watu ninaowapatia mafunzo ya kibinafsi (online) walivyofanikiwa kupata kazi zao kwa mara ya kwanza.

Mfano ni one of my clients yeye nilimpatia mafunzo two days siku ya tatu akaanza kufanya application na akapata “kikazi” cha dollar 10. Note that tulikuwa bado tunaendela na darasa.

Hapa alikuwa anauliza kuhusu payout option anoyoweza kutumia UpWork kupata pesa yake.



Hapo nataka nikuonyeshe kuwa freelancer ndiyo njia ya kuaminika zaidi kujipatia pesa ukifanya kazi Online.

Kwanza kabisa ni rahisi kuanza kujifunza kila kitu unachotakiwa kufahamu ili ufanye kazi zako kwa mafanikio.

Nafahamu there so many people who are struggling to land first job.

Jibu ni rahisi. Kuwa mvumilivu lakini pia fuata sana kila darasa naloandika hapa. Kumbuka kila naloandika hapa si kwasababu naandika tu. Ninachojaribu kushare na wewe ni mambo ninayoyafahamu kwahiyo yanafanya kazi.

It’s for you to choose or ignore.

Sasa tuangalie mambo 5 yakufanya ili utengeneze pesa UpWork 2020.

1 • Apply kazi zile tu ulizo na chance kubwa kuzipata.

Unajua nini.

Kutoka katika experience yangu ninaweza nikakwambia ili upate kazi na kutengeneza pesa inabidi u-apply kazi zile tu unazoweza kuzifanya kikamilifu.

Hii inasaidia sana hata wakati uandika ku-apply hii kazi flow ya uandishi wako itaonyesha kweli wewe unafahamu kazi client anayotaka kufanyiwa.

Nafahamu freelancer wengi wanaoanza wao wana-apply tu kwa pupa. Hii siyo nzuri kwasababu kwanza kabisa unapoteza “connect” (connect ni kiasi cha Point za bure unazoweza ku-apply kila kazi. Sasa ukiwa una-apply tu kwa pupa connect zitaisha bila kupata kazi)

Pili uki-apply tu kila kazi kisa umeona ni pesa nyingi unaweza ukakosa vilevile kwasababu kazi nyingi za pesa ndefu zinahitaji freelancers wenye uzoefu kwamaana wamefanya kazi na wamelipwa angalau $100 inasoma kwenye profile zao lakini pia ni verified.

2 • Hakikisha unakuwa na Skills zaidi ya mbili.

Yes.

Ukiwa na Skills zaidi ya mbili kwa mfano wewe ni translator/transcriber lakini pia ni web developer lakini pia wewe ni graphic designer au pia wewe ni photographer unajiwekea nafasi kubwa sana yakupata kazi.

Kwa mfano juzi nilikuwa naangalia kazi nikakutana na gig ya dollar 500 kupiga picha mitaa ya Dar es Salaam. Na kazi hii alikuwa anatakiwa beginner. Nikasema kazi kama hizi ukiwa smart na unaishi Dar unapata bila shaka kabisa.

Unaona hapo?

Mwaka 2020 kama kweli unataka kutengeneza pesa kama freelancer UpWork basi hakikisha unajifunza Skill nyingine mpya. Na kama unahitaji ushauri katika hili niandikie makingmoneyonlinetz@gmail.com

3 • Ukiwa una-apply kazi dont spend lot of time ukijisifia kuhusu experience yako ya miaka 10. No one cares about that. Onyesha you can do the work instead.

Freelancing site kama UpWork zimeanzishwa kwaajili yakusaidia talents toka duniani kote kupata kazi kwa kuonyesha uwezo wao wakufanya kazi na si miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi husika.

Ndiyo ni advantage kuwa na experience lakini vipi kama experience yako ni outdated?

Hapa ndiyo maana client wengi wala hawakuulizi vyeti vyako. Ukipata kazi utapewa kazi ya majaribio na ukifanya vizuri basi unapata kazi.

Katika threads/post nilizoandika nyuma nimeweka sana wazi kuhusu hii powerful point. Don’t waste kuonyesha you go to university and got your degree. Onyesha you are ready to do the work. And you are going to do right now.

4 • Kuwa active na apply kazi latest tu.

Hii Point ni powerful sana.

Kwa kawaida inachukua siku tatu kwa client kumpatia kazi freelancer.

Sasa wewe ukija kutuma application siku ya tatu ya nne nikwambie tu most likely client atakuwa ameshaanza kuwafanyia interview freelancer waliotuma application mapema.

Sasa hapa unaona client hawezi tena kuwa na muda kupitia application ya wewe mvivu uliyetum siku ya nne mbele wakati kuna freelancer wanaoweza kufanya kazi kama wewe na wametuma application masaa 3 baada ya kazi kuwa posted.

Do you see the point? I hope you do.

5 • Apply kazi zinazotumwa na client walio verify payment account zao.

Ngoja nikwambie kitu. Ili kujiaminisha kwamba client anayetaka umfanyie kazi yupo serous basi atakuwa ama verify payment account yake na pia utaona ameshafanya kazi na freelancer wengine na Amelipa pesa.



Kwa kawaida ukipata kazi kwanza kabisa client ataweka pesa mliyokubaliana katika escrow account. Na utaweza kuona pesa yako kwenye dashboard ya account yako.

Hii ni muhimu kwasababu inakuwa ule uhakika kwamba I’m working with client I can trust.

Pia nimalizie kwa kusema UpWork ni site ya kuaminika

Wewe freelancer na client wote mpo safe.

Yes yes. Leo naomba niishie hapa. Tukutane siku nyingie kwa darasa amazing kama hili.

Cheers
 
Hebu niambie vigezo vya kufanya kazi uko

Soma hapa

Beginner level : Je, Online Freelancing ni nini? Kazi zinatoka wapi? Ni Skills gani zinahitajika? Nitalipwaje pesa? Jifunze kila kitu hapa
 
Nikupongeze kwa kutoa elimu hii ambayo ni mpya kwa watu wengi. Endelea kuelimisha one day yes
 
I'm a physist, can I get as a frr
I'm a physist,can I get job as freelancer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…