Elections 2010 Ultimate Security na Uchaguzi Mkuu

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,429
Reaction score
1,047
Katika vituo tunavyopita hapa Ubungo tunawakuta FFU, POLISI NA ULTIMATE SECURITY. Hivi hawa ultimate lini wamekuwa rasmi sehemu ya dola?
 
Ni miradi ya vigogo wa ccm hiyo...wanagawana hela ya uchaguzi kiaina...uliza baadaye wamelipwa shiing ngapi hao askari, utacheka!
Lakini kwa vile mwisho wao ni leo, acha wamalizie kujikaanga,watazitapika senti hizo!
 
Ultimate tena jamani si kheri mgambo
 
mgambo ni part ya dola,soma sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inapoelezea maana ya neneo polisi! sasa ultimate security mmmh!
 
Katika vituo tunavyopita hapa Ubungo tunawakuta FFU, POLISI NA ULTIMATE SECURITY. Hivi hawa ultimate lini wamekuwa rasmi sehemu ya dola?

ULTIMATE SECURITY ni kampuni ya muasia Tanil Somaiya, yule anayetajwa kwenye ufisadi wa RADA, uagizaji wa magari ya Jeshi n.k. Kampuni yake nyingine ni Shivacom. Labda amepewa tenda ya kulinda usalama wa kura zenu.
 
Hata wangeamua kuwaleta Interpol Mnyika keshachukua jimbo Period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…