Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
JK asipuuzie suala la siasa za Mbeya kama zilivyojionyesha katika chaguzi za kura za Chama kuteua Wabunge.
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa ambayo JK alipata kura nyingi sana hata kuzigi the National average.Mbeya ilikuwa na wastani wa 87-92%
Ukilinganisha na Dar es salaam, kiwango cha kura kutoka Jiji kuu hili lilikuwa CHINI ya kiwango..Dar es salaam ilikuwa na wastani wa 65-75%(National Average 80.28%)
Mivutano iliyojitokeza haimgusi moja kwa moja JK, lakini mteule wake Mkuu wa Mkoa ni mtu aliye karibu sana na mafisadi wasio utakia mema Mkoa wa Mbeya.
Pamekuwapo maoni kadhaa kutaka Mzee Mwakipesile ahamishiwe mikoa mingine ambayo hana mahusiano binafsi kisiasa, hilo halijafanyika.
Siyo siri kuwa RC hana mahusiano mazuri na karibu wabunge WOTE wa Mkoa wa Mbeya.Wabunge hawa wengi wao ambao wamepita kinyang'anyiro cha uteuzi wa kugombea ubunge wanakubalika sana na wananchi mkoani na ni wapinga ufisadi.
Wabunge wawili walioshindwa kinyang'anyiro cha uteuzi wa ubunge, Mama Kilasi wa Mbarali na G Sigonda wa Songwe/Chunya walikuwa na misimamo isiyoelewaka ukilinganisha na wabunge wenzao.Hawa wamebwagwa.
Vile vile Wabunge wa Mkoani Mbeya wameonyesha mshikamano mzuri sana na juhudi zao kisiasa zinakubalika kwa wananchi
Mada hii ni ya kukitahadharisha chama, mahsusi Mwenyekiti wa Chama, JK asipuuzie msimamo wa wananchi ili umaarufu wake usije ukatetereka Mkoani Mbeya, hasa tukielekea uchaguzi mkuu.