Umaarufu wa Kikwete upo juu

Shukran kwa maoni yako. Lakini ni vyema kama ungeiangalia shilingi kwa pande zote mbili, na si kwa mapenzi ya moyo kama ushabiki wa mpira.

Ukweli ni kwamba, wananchi si kama wanamuona Kikwete kama Raisi aliyewatimizia yote, bali wananchi hawawaamini wanasiasa. Na kwa maana hii, hawana imani kuwa kama watambadili na kuuweka upinzani ndio mambo yao yatakuwa mazuri. Maana Zimwi likujualo halikuli likakwisha.

CHADEMA ni moja kati ya vyama vilivyopata heshima sana nchini Tanzania. Lakini tukio la hivi karibuni la kumtoa katika kinyanganyiro cha uenyekiti, mbunge maarufu Zitto Kabwe kimeishushia hadi sana chama hicho. Na wananchi wanajiuliza hivi tukiwapa Urais watawezaje kugawana post za Uwaziri na nyinginezo. Hivi hawa wapo pamoja au wanatuhadaa tu.

Watanzania mpaka leo si watu wa kuchukua Risk kubwa kiasi hicho. Kwa hili wengi tutakubaliana.
 


"rating rate of muungwana zomboka is direct proportional to the illiteracy rate of Tanzanians,".. the more rating yake inavyoongezeka basi ujuwe asilimia ya mabwege Tanzania inaongezeka...upoooo!!!!!.....sasa sijuwi sample size yako umechukuwa wapi!!!

tupe ya makundi tofauti ..na demographic and social economic [and education] status ..then ndio uje kwenye average...hata kama itakuwa asilimia 80% kama mwaka 2005[exclude chamelleon vote papers] then tutajustify majibu hapa ...otherwise kaaa kimya!!!
 
Hapa umekuja na point muhimu sana. Si uongo Vyuo vikuu sikufika na vyuo vya kati sikufika. Nikijua wazi kuwa hawa ndio wasoma magazeti yetu na ndio waliojaa JF.

lAKINI HIYO SIO SABABU KUBWA ILIYONIFANYA MIMI NISIENDE HUKO. Sababu kubwa ni kwamba, inakadiriwa 70% ya watanzania wanaishi vijijini. Na huko ndio mtaji wa CCM siku zote uliko lala. Hata wapinzani hilo wanalijua, ndio maana Makamba kule Tarime alisema kuwa wapinzani sasa wameanza kufuata mbinu za CCM za kuwania kura vijijini. Lakini akajigamba kuwa hii ni kwa chaguzi ndogo tu na isitoshe bado hawana uzoefu.

Hata tukiacha hilo bado wasomi wetu ni asilimia chache, bila kuwapata watu wa vijijini na watoto wa mjini hujafika mbali.

Hivyo bado naona nilikuwa sahihi hata kama vyama vya upinzani vikiungwa mkono na wasomi na matajiri bado si jambo la kutisha sana kwa Kikwete.
 
Shukran kwa maoni yako. Lakini ni vyema kama ungeiangalia shilingi kwa pande zote mbili, na si kwa mapenzi ya moyo kama ushabiki wa mpira.


Watanzania mpaka leo si watu wa kuchukua Risk kubwa kiasi hicho. Kwa hili wengi tutakubaliana.

Mnakubaliana huko madrasa mkuu wakati mkitizama al jazeera na wala sio mtizamo wa watanzania woote.
 

Yap,

Kwa sababu Kikwete atafilisi nchi na kuwafanya wananchi wote wawe katika hali ya umasikini wa kutupwa ili awahonge hata pesa ya chumvi (EPA ndogo aliyotengeza kupitia hii bajeti ya juzi).

Na akiona mambo hayaeleweki, ataleta mahakama ya kadhi na kuibadili TZ iwe nchi ya kiislam (jumuia ya kiislam) so haishangazi kuona ukiwa na confidence kwa Kikwete.
 


Sasa serikali ikiwa ya mafisadi na viongozi wadhaifu una tegemea wata toa waraka wa jinsi ya kupata viongozi bora? Your logic only works if the government has leaders who follow through their promises and honor their oaths of office. Sasa kama viongozi kama hao hatuna wakitoa waraka una tegemea huo waraka uta kuwa vipi?
 
Mnakubaliana huko madrasa mkuu wakati mkitizama al jazeera na wala sio mtizamo wa watanzania woote.

Sasa hayo ni mambo ya wapiga kura, na ndio maana niliwafuata huko. Unajua akili ni nywele na kila mtu ana zake. Na ndio maana tunaita kura ya siri. Na si rahisi mtanzania kukwambia amemchagua nani, kwa maana shida yake yeye wewe huijui.

Mwanamke anapochagua kiongozi, pengine ajenda yake kubwa ni maji. Mwenzangu wa Jangwani pengine ni Mpira, nawe msomi pengine shule. Aliye Ughaibuni pengine uraia wa nchi mbili kama angepewa nafasi ya kuchagua. Mfanya biashara pengine ushuru. Basi hivyo ndivyo demokrasia inavyojengwa katika kuwapata wapiga kura. Hapa ni ilani ndio inafanya kazi.

Tukilazimisha mambo, hapo tutaita mapinduzi. Unaona lugha inavyobadilika.
 
Zawadi, ebu tumia akili yako aliyokupa Mungu just common sense!! kabla ujaweka post yako hivi hiyo research yako umeifanyia wapi au ndo ile kama ya marehemu kolimba iliyokuwa in suggest kuwa watanzania wanampenda Mzee Mwinyi na wanataka abadili katiba na Kuongezewa muda wa kutawala thanks to Mwl,JKNyerere alikuwa bado yu hai!! reseach sio mchezo usikae kijiweni alafu ukatuletea hadithi za nimetembea ujatwambia ulitumia criteria hipi kuuliza uliowauliza hivi ukienda kijijini ukawauliza watu wa masikani ya CCM unategemea kupata majibu yapi!! unasema magomeni sasa kama ukienda magomeni Msikitini /mwembechai ukaoneasha mwongozo wa wakatoliki unategemea nini don't be synical!! God save Tanzanians shameful people like you!! tupe statistics zinazoweza kulegitimaze your so called research otherwise unatia shaka your mental stability usitake nishauri wakupeleke Mirembe hospital!!
God bless Tanzanian na utuepushe na hawa wazushi
 
Mimi ninaamini kuwa Serikali hii, imefanya vizuri sana juu ya kuwasaka mafisadi na hasa katika kuviachia vyombo vya habari huru. Na ukweli ninaamini kbisa kuwa ni lazima twende hatua kwa hatua.

Kwa muono wangu, hatua ya kwanza ni kuwapa wananchi habari. Hapa nazungumzia uhuru wa vyombo vya habari. Hii kwangu ni hatua muhimu sana, ambayo hata akina Zawadi Ngoda tunaweza kuandika bila woga. Eti nikaenda kijijini bila kutumwa na chama au serikali na kuchukua takwimu bila woga. Unajua hata robo ya hayo nisingefikiria wakati wa Nyerere. Hivyo hii ni hatua ya kwanza ambayo tuliikosa hat katika awamu ya Tatu (Mkapa).

Tatizo ikikosekana hatua hii, unaweza kuzungumza jambo la maana sana, na watu wasikuelewe. Mwishoe unaishia kuwatukana watanzania, eti mitanzania imezubaa au mioga au ukatafuta jina lolote lile ilimradi kuonyesha kuwa wewe peke yako ndie unayeelewa. Sasa hili linachukua muda.

Pili ndio kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuwangoa mafisadi. Nilichokigundua mimi kuwa rythm tunayoipiga bado aslimia 70 ya wananchi hawawezi kucheza. Mpaka huo ndio ukweli tutalalama sana na wapinzani tukidhani tunaonewa.

Rome haikujengwa kwa siku moja. Twendeni polepole tutafika tu. Tanzania si nchi pekee barani Afrika yenye matatizo ya kiuchumi, mafisadi na uchaguzi. Si mmeona juzi huko Uganda, wati 14 wameuwawa mjini Kampala.
 
Zawadi, ebu tumia akili yako aliyokupa Mungu just common sense!! kabla ujaweka post yako hivi hiyo research yako umeifanyia wapi au ndo ile kama ya marehemu kolimba iliyokuwa in suggest kuwa watanzania wanampenda Mzee Mwinyi na wanataka abadili katiba na Kuongezewa muda wa kutawala thanks to Mwl,JKNyerere alikuwa bado yu hai!! reseach sio mchezo usikae kijiweni alafu ukatuletea hadithi za nimetembea ujatwambia ulitumia criteria hipi kuuliza uliowauliza hivi ukienda kijijini ukawauliza watu wa masikani ya CCM unategemea kupata majibu yapi!! unasema magomeni sasa kama ukienda magomeni Msikitini /mwembechai ukaoneasha mwongozo wa wakatoliki unategemea nini don't be synical!! God save Tanzanians shameful people like you!! tupe statistics zinazoweza kulegitimaze your so called research otherwise unatia shaka your mental stability usitake nishauri wakupeleke Mirembe hospital!!
God bless Tanzanian na utuepushe na hawa wazushi
 
Hebu soma tena hiyo mistari niliyoiwekea wino mzito. Unajua hili ndilo tatizo lililonisukuma kufuatilia kipima joto. Maana mijadala yote watoa hoja wanatueleza kuwa waraka huo hupatikana kote Tanzania na unaungwa mkono na watanzania wote.

lAKINI PICHA ULIYOIWEKA HAPO NDIO PICHA HALISI, NAMI NAKUSHUKURU SANA KWA HILO, nafikiri wengi watatuunga mkono. Ni kosa kutoa waraka unaohusisha kuchagua kiongozi wa watanzania wote, wakati waraka huo umependwa na watu wa kundi fulani tu. Jamani tufungue macho na kuiona hii hatari. Ikiwa wewe unaelewa hivyo sasa mwenzangu mmachinga asiyeijua hata internate kule Lindi na Bagamoyo utamwambia nini?

Na nimetumia Common sense ndio maana nimefanya hivyo. Hii siiti Research, hili ni neno kubwa kidogo kwa waliokwenda shule wanafahamu tofauti zake. Hii naiita kipima joto, na niliwapima watu laki moja na hamsini elfu tu (Rondom).

Nawe unaweza kufanya sio kazi ngumu sana, hata hapo kijijini kwako au katika mtaa wako. Ni kitu kizuri sana wala hakihitaji shule sanaaaa. Tena tukiwa wengi ndio kazi inakuwa rahisi. Maana wa Mbeya atafanya huko, Moshi vile vile na Mwanza. n.k. Tunaweza kuwaomba hapa JF wakawa na ukurasa huo na tukaripoti kila mwezi.
 

wakuu kama ni pesa za uchaguzi tayari jk anazo juzi wamepiga dola milioni 77 benki kuu[reference The east African 14th sept 2009]..serikali wanajitahidi ku cover wanasema ni dola milioni 5,lakini wameumbuliwa...ni ufisadi mkubwa kama wa EPA....NAsubiri wazee wa upiganaji walinyake.

SO tayari jk anayo pesa ya kampeni mapemaa.....bilioni 100 si mchezo...ana jeuri ya kununua kila kura...kwa pesa hiyo.Tukio la waziri wa fedha kujitahidi ku cover hili suala inaonekana wazi wanajuana na muungwana....na lazima kwanza huyo mkulo aondoke na pesa zetu zilizochotwa TANESCO ,TTCL na makampuni mengine kwa mgongo wa TRA na BOT zirudi!!
 

Anzia wilayani kwako, kisha mkoani na taifa kwa ujumla, tujulishe JK katimiza ahadi gani? Maisha bora kwa kila mtz yamekuwepo?
 

Anzia wilayani kwako, kisha mkoani na taifa kwa ujumla, tujulishe JK katimiza ahadi gani? Maisha bora kwa kila mtz yamekuwepo? Wazee wa iliyokuwa EAC wamelipwa madai yao? Just to mention few!
 

Kweli wewe umelala usingizi! Huyo mtu wa kupambana na ufisadi yuko wapi? Yule anayesema mzee BWM aachwe apumzike? Kama kuna mafisadi wa kupumzika na wengine kuchukuliwa hatua sio usanii huo?
 

Nashukuru dada/mama

Umejibu tena off quote. Yani unacho jibu wewe haihusiani chochote na ulicho quote toka kwangu.

Wewe umesema kuwa haukubali waraka wowote kama hautoki serikalini. Nika kuuliza je kama hiyo serikali imejaa viongozi bora wanaweza kutoa waraka unao hamasisha wananchi tuchague viongozi bora?

Yote uliyo sema kwenye post yako juu yana ukweli ndani yake ila haya husiani chochote na post yangu na wala haija jibu kabisa post yangu.

Shukrani.
 

typical CCM propaganda ... malengo ya "MUULIZE RAIS" hayakufikiwa nini?? ooh i see, now the Lumumba corridors seems to be very busy .... hahaahahaaa .. what a piece of crap!!
 
"Vijiji vya Tabora na Ruvuma, walinieleza kuwa wao ni wakulima wa Tumbaku na toka Kikwete aingie madarakani wamesikilizwa sana kwa kuwabana wawekezaji katika eneo hilo."

Zawadi,
Sema ukweli, propaganda zisikupofue macho. Ulitembelea vijiji gani Tabora? Tazengwa, Lusu, Uyumbu, Kazaroho, , Uyowa au Izimbiri? Hali halisi ya Wakulima wa Tumbaku ninaijua manake Familia yetu ni wakulima wa Tumbaku. Please tell the truth and shame the devil. Ukweli ni kwamba Muungwana ameona umaarufu wake unashuka kwa style ya Free-fall ndiyo maana amekuja na style ya kuongea na wananchi kwa njia ya TV(ambayo nadhani haikuwa na mafanikio) na sasa anawatumia makada wake kwa nguvu kumuuza kwa Watanzania.

Ebu angalia nukuu zifuatazo:-

1. Akitolea ufafanuzi wa kauli hiyo, mtaalamu wa mambo ya tumbaku Profesa Robert Machangu, amesema mkulima hupata hela kidogo sana baada ya kutoa gharama za mbolea, kodi, utayarishaji wa shamba lenyewe, vibarua na kadhalika. Akawaeleza wabunge hao kuwa anachoambulia mkulima wa kawaida ni fedha kidogo tu, tena baada ya kucheleweshewa sana na hivyo wakiachana na zao hilo na kupewa mazao mbadala katika maeneo yao, wanaweza kufaidika zaidi.
SOURCE: Alasiri (29/01/2007)

2. "Mheshimiwa Spika, pia, msimu huu wa mauzo ya tumbaku, sarafu ya Kimarekani yaani dola imeendelea kutumika lakini hadi kufikia sasa malalamiko yamekuwa mengi sana kutoka kwa wakulima kwamba sarafu hii ya kigeni inawachanganya, hasa kutokana na kubadilika kwa thamani ya sarafu hiyo dhidi ya shilingi yetu ya Tanzania kiasi kwamba wakulima wamenituma kusema kwamba hawataki tena kuuza tumbaku yao kwa dola za Kimarekani na kwamba wanataka sarafu yetu ya Tanzania itumike. Katika kufanya hivyo, wametaka uwepo umakini zaidi katika kupanga bei kwa shilingi huku ikizingatiwa bei ya wastani ya dunia. Je, Mheshimiwa Waziri atatoa tamko gani?

Mheshimiwa Spika, kumeendelea kuwepo madaraja mengi sana ya tumbaku kitu ambacho kinaendelea kuwasumbua wakulima katika kupanga tumbaku zao katika madaraja hayo mengi kwa usahihi, huku kukiwa na hisia kwamba wanunuzi hutambua tumbaku zao kuwa za madaraja hafifu na hivyo kutoa malipo duni kwa wakulima, kitu kinachowafanya wabakie katika lindi la umaskini bila matumaini ya kujikwamua kupitia zao hili ambalo linaendelea kuwasumbua wakulima katika kupanga tumbaku zao katika madaraja hayo mengi kwa usahihi, huku kukiwa na hisia kwamba wanunuzi hutambua tumbuka zao kuwa za madaraja hafifu na hivyo kutoa malipo duni kwa wakulima, kitu kinachowafanya wabakie katika lindi la umaskini bila matumaini ya kujikwamua kupitia zao hili. Je, Serikali sasa itaona madaraja haya yakipunguzwa ili yawe machache kama ilivyo katika zao la pamba?
Source: Kikao cha Bunge, seating No. 31, 24 July 2008.
 
Pengine nilijibu kwa mapana sana. Hebu twende hatua kwa hatua.

Kabla sijaenda mbali, hivi hakuna mafunzo ya uraia Tanzania. Unataka kusema mafunzo kama hayo yaliyoandikwa katika waraka huo hayatolewi na Tanzania. Unajua kuwa EU na Marekani zinatoa pesa ngapi kwa serikali kwa ajili ya kuwafundisha wananchi wake Uraia. Hivi Mrema alipokataliwa kwenda Marekani na wamarekani mwaka 2003 walipotoa semina ya maendeleo ya Demokrasia (uraia ukipenda), kwa kigezo kuw yeye ni mzee unafikiri ilihusu nini?

Jamani tuacheni propaganda. Si kubaliani na yeyote anayesema kuwa viongozi wote ni mafisadi. Kwani hawa viongozi ni akina nani. Si ni baba zetu, wajomba zetu, mama zetu, kaka zetu n.k. Mimi ninaamini kuwa tatizo lilopo Tanzania si la viongozi tu, bali ni la watanzania wote. Na tukisimama kuwasaidia viongozi wazuri waliopo madarakani waraka wenye maslahi ya Taifa.

Kwanza nikikukumbusha tu, CCM ni wazuri sana wa kuandika Kuandika nyaraka kama hizo. HATA UKIANGALIA ILANI YAO, utakuta aslimia 85 ya ilani ni muhimili mzuri wa maendeleo kwa Tanzania na wananchi wote kwa jumla, toka kijijini mpaka mjini. Tatizo la CCM linabaki pale pale ni utekelezaji. Na hapa ndipo tunatakiwa tuwaunge mkono na kuwasaidia wale viongozi wenye nia ya kuendeleza Taifa.

Hata kikiingia chama pinzani, tutakuwa tunajidanganya tukifikiri kuwa wote ni wasafi. Bado tatizo litakuwa lilelile, kama hatukulielewa hilo. Ni lazima tuelewe tatizo mama, ndipo tutaweza kuendelea na kutatua matatizo yetu once and for all.

Kwa hiyo skubaliani nawe kabisa pale usemapo "Weweumesema kuwa haukubali waraka wowote kama hautoki serikalini. Nika kuuliza je kama hiyo serikali imejaa viongozi bora wanaweza kutoa waraka unao hamasisha wananchi tuchague viongozi bora?". Kwa sabababu CCM kama wenyewe msemavyo ni wasanii, hivyo ni wazuri sana wa kuandika nyaraka. Fuatilia nyaraka zao za huko nyuma pamoja na ilani yao utaniambia jinsi ilivyopambwa kuwaondoa mafisadi.

Ukisoma vizuri post yangu niliyokujibu mwanzo, utagundua kuwa nilichojaribu kusisitiza sana ni uvumilivu. Nikielewa wazi kwamba hii Demokrasia tunayotaka kuiiga ya ulaya, imewachukua miaka 300 mpaka hapa walipofika. Sasa ya kwetu ni miaka yapata miaka 15 tu. Jamani tuwe na subira na tusiwahadae wananchi, kwa kutumia njia za mkato. Kumbuka: SHORT CUT IN DEVELOPMENT IS A WRONG CUT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…