Umaarufu wa Kikwete upo juu


roho mtakatifu kakuleta huku??????


HAHAHAHAHH!!!!
 
Sehemu kubwa ya maelezo yako na hiyo ripoti, ina ukweli. Napenda kusisitiza kwamba matatizo katika sekta kilimo ni mengi na hakuna jinsi nyingine ni kuyashughulikia tu.

Kwanza ningependa kuwapongeza wakulima wa Tumbaku kwa kufikia lengo la Milenium, yaani kupata 1$ kwa siku
(1300 sh kwa siku). Si nyingi sana lakini ni ahueni. Hata hivyo, binafsi kwa kujua ugumu wa kilimo cha Tumbaku wanatakiwa kupata zaidi ya hapo. Na hayo yote yanashughulikiwa kikamilifu. Safari ni ndefu , lakini la muhimu i kuanza. Na JK ameivalia njuga.

Hiyo ripoti ni ya 2003/2004, nimeifurahia sana. Sasa nakupa kazi moja, yaangalie hayo matatizo yaliyokuwemo katika hiyo ripoti na ulinganishee na hali halisi hii leo. Ukweli utgundua kuwa 50% ya matatizo hayo yametatuliwa. Sitaandika kirefu sana, lakini nitajaribu kukupa picha tu jinsi serikali ilvyokuwa karibu na wananchi katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yao. Napenda ikumbukwe kuwa haya makampuni(kwa mfano DEMON) hayana muda mrefu, yana takriban miaka 15. Na wawekezaji kama ujuavyo wanatusaidia, lakini ni wezi vile vile. Hivyo wanahitaji kubanwa. Ili uwabane ni lazima ufahamu mianya yao ya wizi, na hili lahitaji muda, elimu na uzoefu nao.

Hapa nitakuorodheshea baadhi ya utatuzi wa matatizo yaliyojitokeza: Zao la tumbaku TZ, limeendeshwa katika hali ya monopoly sana. Mkulima hakuwa na uchaguzi wa kumuuzia mnunuzi mwingine zaidi ya wale waliowakopesha vifaa. Serikali imewaamuru kutoa hiyo monopoly. Vipi watafanya hivyo? Kwanza hayo mashirika yatalipwa madeni yao yote waliokuwa wanawadai wananchi. Halafu suala la ukopeshaji wa pembejeo litachukuliwa na serikali. Halafu makampuni yaliyopo, pamoja na makampuni mengine yatakaribishwa katika ununuzi wa tumbaku. Na mwananchi atachagua mwenyewe kuuza tumbaku yake kwa kampuni itayotoa bei nzuri zaidi. Hilo litaanza mwakani na ni habari nzuru kwa wakulima.

Kuhusu Grades, hilo nalo ni tatizo. Wakati mwingine inafikiriwa kuwa makampuni yanfanya mipango na maklasifaya kuweka grade ya chini, pamoja na kuwa tumbaku ina grade ya juu. Wenye makampuni wanadai kuwa , wananchi wangeweza kupata Grade nzuri kama wangeelimishwa. Katika eneo hili kuna utata mwingi. Serikali inampango ufuatao katika kutatua hili.
1. Katika kila kijiji kuwafundisha angalau watu wawili ili wawe kama klasifaya wa wananchi. Pindi klasifaya wa kampuni anaposema hii ni grade I, basi ni lazima klasifaya wa kijiji naye aweke saini, kuwa naye anakubaliana na mchakato huo.
2. Kuwaelimisha wakulima ili wafahamu ni vipi wanaweza kupata grade bora zaidi

Tatizo jingine ulilolisema ni juu ya utoroshwaji wa zao hilo, na kuuzwa Kenya na Uganda. Ukweli mimi binafsi hapa sijaielewa serikali hata kidogo kwa kutokumpa uhuru mkulima kuuza zao lake pale atakapo. Na hii si tu kwa zao la tumbaku, bali ni mazao yote. Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, wakati ambapo mwenye bidhaa yu huru kuuza bidhaa zake kwa yeyote amtakaye na popote atakapo hata nchi za nje. Ina kuwaje leo kumbana mkulima, wakati huo huo muuza pembejeo yupo huru. Kama mkulima amepata bei nzuri Kenya, muache akauze bidhaa zake huko. Katika hili sina mjadala kabisa, na nimelipigia kelele sana. Na nimediriki hata kumuandikia barua waziri wa kilimo/biashara na hata Rais. Kwa bahati mbaya sijajibiwa. Naomba tuungane sote, na tuliombe Bunge letu liondoe sheria hiyo. Serikali ya Kikwete ni yenye kusikiliza wananchi, hivyo tuendelee kuishinyikiza serikali kwani hili lina mantiki.

Ninamaliza kwa kusema, ninaimani kubwa na serikali ya Kikwete kwa vile inasikiliza sana wananchi. Hata wengine wakaipa doa kuwa ni Serikali dhaifu. Eti dhambi yake ni kusikiliza matakwa ya wananchi toaka Pemba mpaka Mbeya, Ruvuma mpaka Mwanza, Waislam mpaka Wakristo, walala hoi mpaka Matajiri na Wawekezaji mpaka Magabachori. Pamoja tutashinda.

N.B Muundo wowote ule wa uchumi usowashirikisha wananchi, utafeli.
 
Unaweza ukajitahidi kum-bomoa mtu kumbe ndio unajenga na kumpandisha chati...!

Uhuru huu haukuwepo enzi zile za Musa (Julius) na che Mkapa, thanx God... watu wanazungumza sasa.

Udini unakutafuna Ng'wana wane. Pole sana.
 

Dada Zawadi nakuunga mkono kwa haya ya kuwa bwana mkubwa amejitahidi hata kwenye mishahara pia imeboreshwa zaidi kulingana na marais wote waliopita. Ila tu angewashughulikia wanaolitafuna taifa kama akina Rostam Aziz (na kundi lake la mafisadi papa a.k.a majambazi wa uchumi wa nchi), jamaa wa makampuni ya madini, wamiliki haramu wa vitalu vya uwindaji, kuwashughulikia Waarabu waliotengeneza nchi yao ndani ya Tanzania huko Loliondo, etc. basi umaarufu wake ungekuwa juu zaidi na tungejiona kuwa tuna rais mzalendo lakini si kwa usanii wake mwingi alio nao kwa sasa.
 
Last edited:

Zawadi,

Tuelezee hayo hapo juu manake hiyo ndo Mirija ya umaskini wetu na ndo inayo chafua umaarufu wake.
 

Mkandara,

Hata nawewe?

Ina maana leo ndio umeanza kung'aka kusema kuwa Kikwete anaandamwa kwa sababu ya dini yake?

Wafuatao wameandamwa sana hapa JF kwa muda mrefu sana:

1. Balali
2. Mkapa
3. Mgonja
4. Mramba
5. Lowasa - unakumbuka kasungura na ndege ya uchumi.

Je hawa wote dini au imani yao ilikuwa uislam?
 
.......

N.B Muundo wowote ule wa uchumi usowashirikisha wananchi, utafeli.

Na hiki ndicho Kikwete anafanya,

badala ya kuwashirikisha wananchi, yeye anawapa utajiri mafisadi waliokubuhu

1. Manji
2. Rostam
3. Waarabu kwenye mbuga za wanyama

Na na na na .... zile trilioni moja alizompatia Peter Noni eti za stimulus (my foot) zilikuwa ni kwa wananchi wapi?
 
yes ni maarufu sana kwa africa kwa kuwa rais pekee asiyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua katika mambo mazito ya kitaifa..............
utafiti wako haueleweki umepatikana kutokana na chanzo/vyanzo gani......
 
Tatizo kubwa la Uffisadi ni maadili mabovu. Tukitaka kuondoa Ufisadi once na for good njia pekee ni kuwekeza kwenye maadili. Kuna njia yamuda mfupi (short term) nayo ni hii ya kamata kamata.

Njia ya muda mfupi nayo inagawanyika mara mbili. Y a kwanza na ambayo ni practicle zaidi na iliyotumika sehemu nyingi duniani katika sehemu zilizokithiri na ufisadi ni Mapinduzi. Kwa kutumia njia hii unaweza kumaliza ufisadi kwa mwaka mmoja tu. Mfano ni kama alivyofanya Jerry Rorling nchini Ghana. Aliwakusanya mafisadi wote na kuwatia shaba. Na kwa Raia wa Ghana yeyote yule atakwambia kuwa wakati wa Rorling kulikuwa na 0 ufisadi, ukilinganisha na sasa wakati wa Demokrasia.

Njia ya pili ni matumizi ya sheria za nchi. Njia hii ni nzuri na inayokubalika duniani kwa nia ya ujenzi wa Demokrasia, lakini inahatari ya kujitengenezea maadui na pengine kuitia nchi katika vurugu. Nchi kama Tanzania ni vigumu kuwapata vongozi wasio mafisadi katika ngazi zote. Sisemi kuwa watanzania wote ni mafisadi, ila hali halisi wote tunaijua. Hivyo Rais Yeyote yambidi awe makini na smart anapolishughulikia suala hili. Katika maswala ya Sheria si lelemama, kama tusomavyo magazetini. Unaweza kukuta hawa watu tunaowataja kila siku kama , Rostam Aziz kumiliki kampuni. Yawezekana majina yao hayapo kwenye usajili wa hayo makampuni, hata kama unajua kuwa hili ni kampuni lake. Mazingira kama hayo yamekutikana pahala pengi sana, kwa makampuni kuandikishwa jamaa au marafiki zao. Kisheria huwezi kumkamata eti kwa vile jana alisema, au nilisikia, au imeandikwa katika JF. Hapo ndipo penye tatizo.

Halafu lazima tuelewe kuwa kuwaweka ndani kwa mara moja watu kama akina Mkapa, Sumaye, Mahita, Balali n.k kwa wakati mmoja, siwezi kupata picha mtikisiko wake. Hata hivyo ni lazima ikumbukwe kwamba, huyu ni rais wa kwanza kulisikiliza Bunge na kumtema waziri mkuu. Mkapa alilalamikiwa sana juu ya aliyekuwa waziri mkuu Sumaye toka akiwa awamu ya kwanza, lakini kwa kuelewa umaarufu wake kwake hakuweza kumtosa. Na kilichofuata ni kumchagua tena kuwa waziri mkuu, na baadaye kumpendekeza kugombea Urais. Hivyo kifupi naweza kusema kuwa huyu amejitahidi, kumbuka hiki ni kipindi cha kwanza tu.

Njia ya tatu na ya kudumu ni kuwafundisha maadili watanzania toka shule za msingi mpaka vyuo vikúu. Hii ni kazi muda mrefu na inahitaji muda na uvumilivu. Hii itwawezesha watanzania kukanyana toka kwenye familia zetu. Tusifurahie kuona baba ni Daktari na wala hana mradi mwingine, lakini anajenga jumba la milioni 200 Mbezi na tukafurahia tu. Ni lazima katika mazingira kama haya watoto, makaka, wajomba waweze kumuuliza hivi mwenzetu unafanyaje mpaka unafanikisha haya? Kuwepo na uchungu wa kuelewa kuwa hizi ni fedha za wagonjwa. Haww mafisadi si watu toka Uingereza, Ngeria au Misri, bali ni ndugu zetu watanzania, ni mimi na wewe. Fisadi hana alama wala rangi.

Mimi nimeridhika kwa hatua aliyoipiga ya kuanza au kuonyesha nia ya kushughulikia Ufisadi. Safari bado ni ndefu sana, tena sana, lakini cha msingi ni kuwa na moyo na nia. Nchi ambayo kwa zaidi ya miaka 30 watu walikuwa wakijichukulia tu bila kuulizwa, leo mnataka alitatue tatizo hilo kwa miaka mitano. Nchi ambayo haikutenganisha kati ya serikali na chama, na ikaenda mbali zaidi kwa kauli za "chama chashika hatamu". Maana yake chama chukua tu bila mahesabu, kwani huu si ufisadi. Haiwezekani!

Tuwe na subira, na pamoja tutafika tu kwa sababu, Nia ya kuutokomeza ufisadi tunayo, Sababu za kuutokomeza ufisadi tunazo, Na nyenzo za kuutokomeza ufisadi tunazo. Sasa twende kazini, Kikwete anaweza.
 
Tuwe na subira, na pamoja tutafika tu kwa sababu, Nia ya kuutokomeza ufisadi tunayo, Sababu za kuutokomeza ufisadi tunazo, Na nyenzo za kuutokomeza ufisadi tunazo. Sasa twende kazini, Kikwete anaweza.

Kikwete hawezi kupambana na ufisadi dada Zawadi. Sababu hasa ni kwamba, CCM inafadhiliwa na hawa mafisadi na hasa wakati wa uchaguzi. Sasa unategemea fisadi akikupa pesa zake unatarajia yeye atazirudishaje pesa alizokupa? Maswahiba wake ambao pia ndo wanaoratibu kampeni za kumuweka madarakani ndo hao mafisadi wakubwa unategemea nini hapo? Unategemea kuwa anaweza kuwageuka? Thubutu. Kwahiyo Tanzania chini ya Kikwete tutarajie kuendelea kuumia tu na rasilimali zetu kuzidi kuporwa.
 
Hata mimi kwa vipi tena?... yaani unataka kusema siwezi kuona udhaifu wa hoja zilizopo hapa au?
Na wewe hao umewatolea mfano kwa sababu ya dini zao au!, mbona sioni jina la Muislaam au Baniani...huu ndio Udini wenyewe nao zungumzia..kwamba unaandika hoja inayotenganisha watu ktk makundi yao ya dini badala ya mabaya yaliyofanywa na watu hao kuwatenganisha na wengine.
Nitarudia kusema kwamba makosa ya mtu hayana dini ila mnapozungumza ya Kikwete na dini zikatumika kuelezea hoja nyingi bila shaka kuna udini.
Hakuna mtu alohoji dini za watu hao wala imani yao na hata siku moja sijawahi kuona mkristu alofanya Ufisadi dini yake ikawa somo la ufisadi wake. lakini kwa JK nimeona mengi sana yanaytomhusisha yeye na dini yake kama vule JK angekuwa Mkristu au dini nyingine isingekuwa ktk mtazamo huo.

Huyu jama kaleta hoja ya umaarufu wa Kikwete, wewe unapinga umaarufu huo, andsika vigezo vinavyokusukuma useme kuwa sivyo badala yake naona maswala ya waraka, sijui Uchumi wakati nchi yetu haijawahi kuwa na uchumi mzuri..na wala sababu hizo zisitumike ktk umaarufu wa mtu. Mkuu binafsi naamini kabisa Kikwete ana umaarufu mkubwa sana na kosa wala sii lake ila sisi wananchi wenyewe kwa sababu kiongozi bora kwetu ni yule mwenye sifa tunazozifikiria sisi wenyewe...
 
Ukweli ni lazima ni kiri, kuwa sijui lolote juu ya pesa zitumikazo kwenye chaguzi kwa vyama vyote zaidi ya zile Ruzuku toka serikalini. Ni dhahir kabisa kuwa ukiangalia matumizi wakati wa uchaguzi, ni makubwa sana kuliko hiyo ruzuku kwa vyama vyote.

Kwa mfano, nashindwa kuelewa CHADEMA ilipata wapi pesa ya kumtembeza Mowe kwa Helkopta Tanzania nzima wakati wa uchaguzi 2005. Jeuri hii hata CCM wenyewe hawakuwa nayo. Halikadhalika nikashangaa vile vile ni vipi CCM inaweza kugawa kanga, sukari na takriban kwa wapiga kura Tanzania nzima kwa kipindi cha karibu miezi miwili. Hapo twasikia tetesi tu, mara hawa wamepata fedha toka kwa mafisadi na wao wakikituhumu CHADEMA kwa kupata pesa toka nje na n.k. Ok, sijui nani anasema kweli. Tatizo hatuna sheria katika hili, hivyo kila mmoja anfanya kama awezavyo.

Tukichukulia marekani, wenzetu wameweka sheria kabisa iliyokuwa wazi katika maeneo yote. Hata wale matajiri wana kikomo cha mchango wanchoweza kutoa kawa chama. Vile vile ni marufuku kupata mchango toka nchi za nje. Na sheria nyingine nyingi tu. Cha msingi zipo sheria ambazo zinawalinda. Isitoshe wakati uchaguzi unaendelea tunataarifiwa kiasi cha pesa zilizotumika, nani anakaribia kufilisika na nani amepata pesa kinyume cha sheria. Na hata mgombea anaweza kuwekwa pembeni ikiwa amepata pesa katika njia isiyo halali.

Wakati umefika sasa kwa Tanzania nao kuwa, na sheria na ufuatiliaji na kuvidai vyama viwakilishe mapato na matumizi yao ikiwezekana kila siku au kila wiki wakati wa uchaguzi. Nafikiri wananchi wangependa kujua kuwa ni kiasi gani cha pesa CHADEMA kilitumia kwa Helkopta tu mwaka 2005. Maana CCM iljaribu kuiga katika uchaguzi mdogo kule Tarime, lakini kwa kuona utobokaji wa mfuko, Makamba aliwajibika kupiga marufuku matumizi ya Helkopta kwa siku za usoni.

Hivyo ukiniambia kuwa CCM walitumia fedha ya mafisadi, hilo siwezi kujibu si kwa CCM, CHADEMA au CUF. Ninachoweza kusema ni kwamba, mpaka sheria mahsusi hazijawekwa juu ya uchangiaji wa chaguzi kwa vyama uvunjwaji wa sheria utatokea kwa vyama vyote. Wakati umefika wa kuweka hizi sheria. Cha kusikitisha, Bunge wala halijazungumzia hili kitu ambacho mimi nilifikiri ni muhimu sana hasa ukizingatia tetesi za fedha za EPA na Uchaguzi 2005.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…