The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Kastori karefu lakini katamu, hivi unajua Ferguson alikataa katakata usajili wa Vidic?
Sikia hiii.....
Moja kati ya mabeki ambao Sir Alex Ferguson alikua anawakubali ni Steve Bruce, hata baada ya Bruce kuondoka United mwaka 1996. Ferguson alipenda sana kupata beki mwingine mwenye kariba ya Bruce.
Mwaka 2002 maskauti wa United walimpa taarifa Ferguson kwamba wamemuona kijana mdogo aitwae Vidic anaye kipiga huko Serbia kwenye Klub ya Red Star Belgrade, na maskauti walimpa taarifa kwamba kijana huyo ana sifa kama za Bruce kama ambavyo Ferguson alikua anapenda.
Baada ya Ferguson kupewa taarifa zile alipenda sana kumuona Vidic ili kushuhudia kweli kama ana sifa
kama za Bruce. Mwezi wa 11 mwaka 2002 kulikua na mechi ya kirafika kati ya France na Serbia, Ferguson alipopata taarifa hiyo akaamua kusafiri hadi ufaransa ili kuona mechi hiyo kusudi amshuhudie Vidic uso kwa uso.
Kwenye mechi ile Vidic alicheza kama "Man marker" (wachambuzi watatuelezea zaidi hapo), yaani kazi
yake ilikuwa ni kumkaba mtu mmoja tu (Henry). Ferguson anasema majukumu aliyopewa Vidic kwenye mechi ile yalimfanya asione ubora sahihi wa Vidic kwani United ilikua haichezi na "Man marker", kwa hiyo aliona Vidic asingekua chaguo sahihi kwake.
Baada ya mechi ile Ferguson akawaamuru maskauti wake waachane na Vidic waendelee kutafuta wachezaji wengine. Vidic alikipiga Red star hadi alipojiunga na Spartak Moscow mwaka 2004. Alipokua Spartak Vidic aliimarika maradufu, timu zote kubwa za Ulaya hasa za Italy zilimtolea macho.
Mwaka 2005 mbio za kumsajili Vidic zilikua zinaongozwa na timu tatu, yaani Man United, Liverpool na
Fiorentina lakini Fiorentina ndiyo wakashinda mbio hizo. Kumbuka wakati huo Fiorentina ndiyo walikua Man city
ya Ulaya, yaani walikuwa wanamwaga hela.
Tarehe 22 Mwezi wa 12 mwaka 2005 Fiorentina walikubaliana kila kitu na Spartak Moscow na Vidic mwenyewe ili dirisha la Januari Vidic ajiunge na Fiorentina. Makubaliano yalifikiwa pande zote, ikawa inasubiriwa tu dirisha lifunguliwe ila usajili ukamilike.
Kwa wakati ule Italy kulikua na sheria inayo dhibiti idadi
ya wachezaji wanao takiwa kusajiliwa ambao wanatokea
kwenye nchi ambazo sio mwanachama wa umoja wa
ulaya (EU), kwa wakati ule Serbia hakua mwanachama
wa EU na tayari Fiorentina ilikua ishafikia idadi inayo takiwa
kwa hiyo ikabidi Fiorentina ijaribu kupunguza mchezaji
mmoja ili Vidic aingie.
Baada ya Spartak Moscow kuona Fiorentina wana suasua kukamilisha usajili wa Vidic ikabidi wamrudishe
Vidic sokoni. Liverpool waliposikia habari hizo wakaanza mazungumzo moja kwa moja na Spartak Moscow na
kwa wakati ule Liverpool walikua kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Vidic.
Baada ya Vidic kuona usajili wake umeshakuwa na sinto fahamu, ikabidi aongee na viongozi wa Spatak kuhusu hatma yake na kuwaambia kwamba anataka kwenda United. Kumbuka wakati huo United walishajitoa kabisa
kwenye mbio za kumsajili.
Ferguson aliposikia habari hizo akawaambia viongozi wa Spartak Moscow kwamba, wako tayari kumsajili Vidic lakini bahati mbaya mchakato wa kukamilisha usajili huo ulikuwa taratibu mno kutokana na United walishajitoa kwenye dili hilo.
Kwahiyo mazungumzo yakaanza upya na pia United ndiyo ilikua inaingia kwenye utawala mpya wa Glazers, kwa hiyo bado uongozi ulikuwa haujatulia vizuri. Baada ya kuona hivyo Liverpool wakawa na uhakika kwamba dili hilo litakufa na watamnyakua Vidic.
Ferguson baada ya kugundua hilo akaomba Spartak wamruhusu Vidic aje England kwani amemualika kula Krismasi nyumbani kwake, kwa wakati huu United wanajipanga kukamilisha usajili wake. Basi unaambiwa siku ya Krismasi Vidic alipofika tu jijini Manchester Ferguson akampa jezi, wakashika wakapiga picha na
kuwaambia Manchester United watangaze kwamba wamemsajili Vidic. [emoji23]
Kitendo kile Spartak Moscow hawakukipenda kwasababu dirisha lilikua halijafunguliwa na makubaliano yalikuwa hayajafikiwa kwa 100%. Baada ya mvutano wa hapa na pale ndipo wakafikia makubaliano ya ada ya £7m na baada ya hapo Vidic akafanyiwa vipimo na dirisha lilipofunguliwa akasajiliwa rasmi. [emoji23]
Vidic ndiyo alikuwa usajili wa kwanza United chini ya utawala wa Glazers. Akiwa United Vidic alitwaa EPL mara 5 na kuwa mchezaji bora wa msimu mara mbili 2008/2009 na 2010/2011.
Happy Birthday Vidic