Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Nikikumbuka zoezi la mchakato wa awali la usaili kwa ajili ya ajira za TRA lilivyochukua muda mrefu nikaamini zoezi hilo lingekuwa na umakini mkubwa lakini sivyo zoezi hilo liligubikwa na uzembe, ufisadi na rushwa.
Katika hali isiyitarajiwa kijana mmoja alijikuta akiongea kwa uchungu na kusema angekuwepo Magufuli haya yasingetokea, waliokuwepo karibu yake wakataka kujua kulikoni?
Kijana akaelezea na kusema, namnukuu"nilikuwa ni moja wa walioomba ajira za TRA lakini nimeenguliwa na sababu sikupeleka Vyeti kuwa certified na mwanasheria. Akamaliza kwa kusema vyeti nimepeleka kuwa certified vyote na ushahidi akaonesha"
Huyo ni moja ya waliokumbwa na hali hiyo ambayo naweza kusema ni uzembe na nyuma yake kuna rushwa na ufisadi. Katika hali ya kawaida zoezi la mchujo wa awali halikutakiwa kugubikwa na kasoro kama hizi ikizingatiwa lilitumia muda.
Yaweza kuwa ninayosema sasa ni historia kwa ajira za TRA lakini ili kudhibiti haki za masikini kuporwa kwa uzembe kwenye michakato mingine ya ajira inabidi wahusika wawajibike.
Sasa hivi utumishi imekuwa chaka la ukandamizaji wa haki za masikini waliosoma kwa tabu na wanapata tabu zaidi kushindwa kuajiriwa si kwa sababu ya kupungukiwa sifa ila kupunguziwa sifa.
Nilipokuwa katika kutafakari hayo ghafla ikanijia taswira ya Hayati Magufuli akipambana na uzembe, ufisadi na rushwa na zaidi nakumbuka alipokuwa anasisitiza rushwa ni adui wa haki Leo ndio tunashuhudia utumishi na kwingine, haki za masikini zikiporwa.
Licha ya kutokuwepo Magufuli lakini Umagufuli tuuenzi, hiyo ndio silaha ya wanyonge kupata haki zao.