Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 262
- 361
Habari wanajamvi.
Leo nimewaza sana na kujiuliza sana umuhimu wa waliobobea katika sayansi ya jamiii wako wapi? Na mchango wao katika jamii ni upi?
Sisemi kwamba hawa wataalamu hawajafanya chochote hapana, lakini kwanini Kuna matatizo sugu ambayo wanaweza kuyashughulikia lakini mpaka leo yapo tu.
Nimewaza haya na kujiulizi hivi Kwasababu zifuatazo:-
1. Kama kweli wapo wabobezi hawa kwanini matatizo katika jamii, serikali,taasisi/mashirika hayaishi?
2. Kwanini mchango wao umeshindwa kuonekana moja kwa moja hasa katika matatizo yaliyozoeleka na yanayojirudia rudia kwa miaka mingi iliyopita. Mf. Matatizo ya mfumo wa uongozi, demokrasia, utamaduni, maadili, umaskini, changamoto za usawa na ubaguzi uzalendo na n.k
Baada ya kujiuliza mambo hayo na mengine mengi nimewaza kwamba Kuna haja kubwa sana ya kurejea mifumo ya mababu zetu waliyokuwa wakitumia ili tupate msingi mzuri na baadae tuboreshe mifumo hiyo kwa maarifa ya sasa ili twende vizuri na hatimae tufanye kila kitu katika misingi ya tulikotoka inayokidhi mahitaji yetu kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya sasa.
Na pia nimewaza kwamba serikali yetu kwa kushirikiana na wataalamu wote wa sayansi ya jamii, watafiti, wazee wa kimila, machifu na viongozi wa kijamii washirikiane kuandaa mpango mahsusi wa kubadili mtazamo huo.
Na mwisho kabisa, serikali ijitahidi kufikia makundi yote muhimu kuanzia taifa, Kanda,mkoa,wilaya, halmashauri, kata, mitaa na vijiji ili watoe maoni yao katika mchakato wa kuanda dira ya maendeleo ya taifa 2025-50, na izingatie mchakato huo kwakua ndio njia pekee ya kuifanya Tanzania nchi ya Aina yake inayokidhi matakwa ya wanainchi,serikali, mashirika, taasisi zetu na inayoendana na kasi ya maendeleo ya Dunia kwa ujumla.
Kiraka