Umakini uwepo ujenzi wa madarasa kupitia wakandarasi

Umakini uwepo ujenzi wa madarasa kupitia wakandarasi

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Maeneo mengi ya nchi wameamua kutumia wakandarasi kujenga madarasa kutokana na pesa zilizotolewa mkopo na IMF. Lakini pamoja na kutumia wakandarasi baadala force account Iliyokuwa imezoeleka umakini unahitajika vinginevyo tutapigwa na madarasa haya yatajengwa chini ya kiwango.

Ujenzi wa madarasa kupitia force account ulikuwa mzuri sana na madarasa yalijengwa kwa ubora mzuri kutokana na usimamizi mzuri wa kamati na halmashauri.

Local fundi kwenye force account walijitahidi kujenga kwa ubora kuepuka kuambiwa wabomoe warudie kazi, na si hivyo kila hatua ilikuwa ni lazima wakaguliwe ndio waende hatua nyingine.

Lakini hii ya kutumia wakandarasi kujenga madarasa kila kitu wanunue wao, na kila kitu wafanye wao na kukabidhi jengo kwa milioni 20, pamoja na kununua viti 40, kuweka tiles, milango ya mirunda au mkongo, madirisha ya aluminium tujiandae kuwa majengo ya chini ya kiwango.
 
Swala la chumba kimoja kikamilike na madawati kabisa kwa Tsh20M kwa kila darasa ni la kitaifa au liko applied maeneo tofauti tofauti???
 
Wakandarasi na mchakato wa kuwapata ni pasua kichwa. Tena haina maana kua mkitumia utaratibu huo hamtapigwa.

Tangaza tender utaona vituko. Darasa moja kila bidder anakuja na bei yake tena tofauti zinakua kubwa sana. Mwingine anakuja na 37mil kwa darasa moja wakati mwingine anabid 48mil!

Kwa uzoefu wangu 20mil inatosha ujenzi wa darasa. Ni bora watumie force account maana kwanza wanawawezesha ma local fundi has a ukizingatia ubora wa kazi ni uleule. Wakati mwingine wakandarasi wanakua wasumbufu saana sana hasa kukamilisha mradi kwa wakati
 
Back
Top Bottom