Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UMAR ''SIMBA WA JANGWANI'' MUKHTAR
Umar Mukhtar akiwa kafungwa minyororo baada ya kukamatwa
Siku kama ya leo tarehe 16 Septemba 1931 ndiyo siku Umar Mukhtar alinyongwa na Wataliani baada ya kupigananao kwa miaka 20 akipinga ukoloni wao.
Mara ya kwanza kuiona movie ya ''Lion of the Desert,'' kuhusu maisha ya Umar Mukhtar ilikuwa mwaka wa 1989 niko ndani ya basi natoka Khartoum nakwenda Jazeera mji kusini ya Khartoum.
Movie hii iliyochezwa na mabingwa wa uigizaji ilichezwa na Anthony Quinn, Oliver Reed na Irene Papas kwa kuwataja wachache.
Movie hii ilitengenezwa na Mustafa Akkad ambae pia ndiye aliyetengeneza ''The Message,'' maisha ya Mtume SAW.
Mustafa Akkad aliuliwa mwaka wa 2005 Amman Jordan ndani ya ukumbi katika sherehe ya harusi katika shambulizi la kigaidi.
Niko ndani ya basi zuri la kisasa kiyoyozi kinanipiga katika jua kali la Sudan.
Barabara nzuri sana na nikiangalia nje vijiji tunavyopita kila nyumba nje kumeegeshwa tractor kuonyesha kuwa hizo ni sehemu za wakulima.
Kabla ya kufika Sudan nilidhani ni nchi masikini lakini nilipofika nilijionea kwa macho yangu mwenyewe kuwa haikuwa hivyo.
Wakati naangalia hii movie ya Omar Mukhtar mafaili yakawa yanafunguka inanijia movie nyingine niliyoiona nikiwa mtoto mdogo nimeongozana na baba yangu Everest Cinema, Moshi mwaka wa 1964,'' Khartoum,'' historia ya Mahdi wa Sudan alivyopambana na Gordon Pasha vita alivyovianza dhidi ya wakoloni wengine Waingereza akitokea kwao Jazeera nilipokuwa naelekea.
Hii movie ''Khartoum,'' imechezwa pia na waigizaji wakubwa wa nyakati zile, Charlton Heston na Laurence Olivier.
Siwezi kuhesabu ni mara ngapi nimeziangalia movie hizi katika maisha yangu kwani hazinishi hamu kiasi nimewaambukiza hadi watoto wangu kwani na wao hizi movie zipo katika orodha zao za, ''All time classics.''
Mahdi ndiye alikuwa Khalifa wa Ansar jeshi la Waislam dhidi ya wavamizi wa Kiingereza na Wamisri waliotokea Misri wakishirikiana na watawala vibaraka wa nchi hiyo katika miaka ya 1800.
Ansar walitambulika katika uvaaji wa kanzu zao fupi zilizokuwa zimepigwa viraka vingi.
Katika historia ya Umar Mukhtar ninapoiangalia movie yake huwa nafungukiwa na mafaili mengi ndani ya kichwa changu.
Namuona Sheikh Hassan bin Ameir ambae na yeye kama Umar Mukhtar alikuwa mwalimu akisomesha Qur'an na wazalendo hawa harakati zao za kupinga ukoloni zimepishana kwa miaka 30 tu ambayo ni miaka midogo sana katika historia.
Wote walikuwa waalimu wa madrasa na wote walipigania uhuru wa nchi zao.
Umar Mukhtar amenyongwa mwaka wa 1931 kwa ''kosa,'' la kuipigania nchi yake.
Umar Mukhtar alikuwa Khalifa wa Tariqa ya Senussi na kiongozi wa zawiyya.
Sheikh Hassan bin Ameir ameingia katika siasa mwaka wa 1950 akiwa Khalifa wa Tariqa Quadiriyya akija katika TAA na baadae TANU na jeshi kubwa la murid nyuma yake kutoka zawiyya kadhaa zilizokuwa Tanganyika na hawa ndiyo waliokuja kuwa wanachama wa mwanzo wa TANU na wengine kama Sheikh Mohamed Ramiya wa Bagamoyo na Sheikh Yusuf Badi wa Lindi wakaja kuwa viongozi wakubwa wa harakati za uhuru chini ya Sheikh Hassan bin Ameir.
Ukipitia maisha waliyopitia wazalendo hawa utasema kama ingekuwa ni kitabu cha maisha yao mfano wa riwaya basi utadhani mwandishi wa riwaya hizo ni mmoja kwa jinsi zinavyofanana.
Hii ni kuanzia kusomesha, ucha mungu wao, umasikini, kusalitiwa na ule moyo wa kujitolea kwa nchi zao lau kama Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa Mzanzibari aliyepigania uhuru wa Tanganyika.
Umar Mukhtar alikwenda hadi Chad kupambana na ukoloni wakati Sheikh Hassan bin Ameir alifika hadi Malawi Congo ya Mashariki, Rwanda na Burundi na kote huko aliacha wanafunzi na zawiyya na hawa ndiyo waliompa shida sana Mbelgiji.
Picha: Picha za kukamatwa Umar Mukhatar na kunyongwa kwake na jeneza lake likiwa mabegani mwa watu wake hazihitaji maelezo kwani zinajieleza.
Picha mbili za mwisho ni Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Umar Mukhtar wakiwa katika umri wa miaka 70 na kitu.
Angalia jinsi walivyofanana kwa namna ya ajabu sana.