Umasikini na ongezeko la mishahara

Umasikini na ongezeko la mishahara

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
masikini ni yule anayejitahidi kutokuonekana masikini.
  • Akipata 10000 akanywee pombe 7000, elfu 3 anunue vocha na chai kesho yake
  • Akipata elfu 5 anunue chakula cha elfu 3, vocha mia 5 na hela ya daladala

Hali hii ipo wired kwenye akili za watu katika makuzi. Umezaliwa hivyo na utakuwa hivyo mpaka mwisho wa maisha yako.

Simulizi kutoka AtlantaFX : Series 1 Episode 4 ( The Streisand Effect)
Ernest na Darius wanaenda kwenye duka la mkopo(pawn shop); unaweka bidhaa unapewa hela utakayo lipa kwa riba ili ukomboe bidhaa yako au ubadilishane bidhaa kwa bidhaa.
Ernest ana simu anataka dola 200 zimsaidie kuendesha shughuli. Darius akamwambia kama anataka hela zaidi achukue jambia (katana) atamsaidia kupata hela nyingi.
Ernest akakubali kuchukua jambia.
Darius akampeleka Ernest kwenye ghala lina watu wa asili ya asia. Ghalani Darius akawapa watu wale jambia nao wakampa mbwa aina ya Cane Corso.
Darius akamchukua Ernest wakaondoka wote kuelekea eneo la kijijini.
Kufika pale wakakutana na bwana shamba mmoja, Darius akampa bwana yule mbwa na kugeuza kuanza kurudi alipotoka.
Ernest akaduwaa na kuuliza "hela vipi?"
Darius akasema " Atatupa baada ya miezi 6, yaani atamchukua huyo mbwa ampandishe kwa mbwa wengine, vile vimbwa vitakavyozaliwa vitauzwa kwa dola 2000 kila kimoja na wewe utapata nusu ya mapato yote".
Ernest akajibu, "mimi ni masikini, sina muda wa kuwekeza. Nafanya juu chini ili nisiwe masikini. Ninahitaji hela sasa hivi hata iwe ndogo kiasi gani"
canecorso.jpg
 
Sijui kwanini, yaani siku zote Wafanyabiashara uchwara na Jobless VITA yao kubwa sana ni WATUMISHI ( Walioajiriwa ).

Jamani kila mtu aiishi Maisha aliyochagua.

Kama wewe unaishi Maisha mazuri sana kwasababu hutaki UTUMWA na utakuwa TAJIRI. Good for you!

Achana na waajiriwa, waliokubali kuwa watumwa na masikini waishi Chaguo lao.

Screenshot_2022-05-03-16-13-06-554_com.twitter.android.png
 
"mimi ni masikini, sina muda wa kuwekeza. Nafanya juu chini ili nisiwe masikini. Ninahitaji hela sasa hivi hata iwe ndogo kiasi gani"

Kuna watu wana Akili alafu kuna wale akina sisi wenye Maarifa. Kila mtu anahitaji mtu wa kumtoa alipo na ampeleke sehemu nyingine haijalishi ni kwa gharama gani.
 
Mwisho wa siku wote mtakufa Sasa yanini shida na mateso duniani life is too short na ujuaji ujuaji ni ugonjwa so watch out
 
Back
Top Bottom