Umasikini ndo unasababisha tufanye sensa za Mikingamo, wenzetu wanajua hata kama ukilala njaa

Umasikini ndo unasababisha tufanye sensa za Mikingamo, wenzetu wanajua hata kama ukilala njaa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Natamani kuona kila mtu akihesabiwa kwa maendeleo sawa ya nchi yetu.

Ila bado nailaumu Serikali na NBS kwa kulifanya lionekane swala la Kisiasa.

Wameshindwa kutumia Teknolojia kufanikisha hili swala kwa 50% siku ya kwanza badala yake siku ya kwanza wanaenda kufanyiwa Sensa watu 9%.

Kwanza hawajatoa Elimu ya kutosha kwa Wananchi. Watanzania wanaamini kuwahesabu ni kuwachulia kifo, hatoi namba sahihi.

Pili sehemu za Mijini wangetumia Application za simu ambazo mtu naweza kujaza ile fomu yake hata kama yupo ndani ya basi anasafiri.

Pia miezi miwili kabla walitakiwa wawe wameshasambaza maswali wanayouliza ili watu wajiandae, eti leo mtu anaulizwa namba ya NIDA, kweli?

Wanasiasa wa CCM wiki mbili za mwisho kutumia Mgongo wa Sensa kujitangaza ndo imefanya ionekana ni swala la CCM. kumvuka wanachama wa CCM hawazidi Mil 10 kati ya Watanzania Mil 60.

Serikali ilishindwa kutumia Mitandao Mikubwa kama JamiiForums kutoa elimu ya Sensa, wanaishia hela kuisambaza kwa Wanavikundi wa CCM Wafanye Mabonanza na maonesho. Hakuna hata mmoja alofanya onesho wala Bonanza Vijijini.


Hii kazi ingefanywa na Walimu kuliko kuwapa watu wasiojua hata kutumia tablets. Watu wa Sensa wamepewa nafasi kulipana fadhira

Je, kwanini Serikali haijatumia Teknolojia kufanya Sensa?

Kwanini Wametumia wana CCM wawe Makalani wa Sensa? Wananchi hawaongei ila wanajua.

Pamoja na mapungufu yetu, bado Sensa ni Muhimu kwa Nchi ili kutoa huduma sawa.

Chonde chonde, kubali kuhesabiwa

Sensa si ya Samia wala Mbowe bali ya Watanzania
FB_IMG_1661248058842.jpg
 
Tz waambie kuiba kura. Fastaaaaa..

Hiyo NBS ni bure. Nilitegemea Website yao iwe na data A to Z za nchi. Tena Real Time.
 
Ili swala la sensa wangepita kupitisha karatasi jana siku moja kabla kwa kila kaya. Ambayo wangetumika kuijaza asubuhi. Then karani angepita kuhakiki na kuhoji palipo na upungufu ndio anajaza taarifa.

Sasa sensa ya siku 3 kutakua na mkanyagano wa taarifa si wote watakumbuka taarifa za siku 3 nyuma. Wengine watasafiri katikati hapo ata famili nzima.
 
CCM haujawahi kufanikiwa kwa jambo lolote.

Hata uchaguzi huwa wanaangukia pua, sema huwa wanabebwa na vybo vya dola tu.
 
Back
Top Bottom