Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Acheni mashala nchi ilikuwa sahihi kabisa, huo ndo ujamaa na kujitegemea unao takiwa, si mliukubali? Unalialia humu nini sasa
huo ni unafiki

Tatizo wabongo mwapenda dezo za nchi za wanaume wa kizungu kirahisi mnoo. halafu mnaogopa dezo za wake zenu matajiri eti mke tajiri ana nyanyasa...mbona hamueleweki?

hamna viwanda vya kutengeneza bidhaa mnazo taka. anzisheni vyenu, ili weupe nao waige, ambapo ndo Julius alilenga twende kiviwanda viwanda..alisema '' tufunge mkanda'' mkashangilia! sasa je
kwani leo mna raha gani? Bongo leo maji mwanywa ya visima vifupii vya mavi ,hamna kazi,elimu duni tu, UDA ,VIWANDA mmeshindwa nk,
usijiangalie wewe tu,angalia wlio wengi

kuhusu mke wa mtu kutembea na mgambo. hata leo wanapigwa na boda boda sana. na wauza magenge siyo wote lkn wengi.
Naenda zangu mie!
 
 
Miss, Naona kuna mambo umechanganya.
 
Kwa nchi kama hii inayotegemea misaada/mikopo ktk ku-finance bajeti yake unapokuwa na kutokuelewana na hao wakopeshaji wakubwa kama IMF/WB hata wale washirika wengine wa maendeleo hawawezi wakakustai.

Ndio maana watakusukuma tu kukurudisha kwao. Nakumbuka nchi kama Nigeria kwenye 1980s walihangaishana sana na IMF hadi serikali ya kijeshi ya wakati ule ikaamua kuupeleka mjadala wa aidha kuyakubali masharti ya IMF au la kwa wananchi ambao waliyakubali kupitia "Referendum".

Ndio maana kwa nchi kama Tanzania kushindana na hawa watu inakuwa "Detrimental" kwetu kwani hatuna njia mbadala.
 
Mpaka lini??
 
Mku kauli mbaya siku zote huwa zinaharibu uhusiano na kumbuka hawa jamaa hawa cha kupoteza na ikiwezeka wanaweza vilevile kuotesha utawala wao na kuweka imaya yao.
Kuna namna ya kula na mtu bila kumshika mkono
 
Kwa kweli naona kuna baadhi ya wachangiaji wako mbali kabisa na historia ya nchi yetu, nitasikitika sana kama miongoni mwao watakuwa ni watu wenye viwango vya Usomi wa Shahada za chuo kikuu.

Kwa wale wasiofahamu ni kwamba Mwalimu alitaka kuondoka madarakani mwaka 1975. Lakini wazee wa CCM wakiongozwa na Sheikh Thabit Kombo walimuomba mwalimu abakie kwa kuwa Mwaka 1972 walitoka kumpoteza Mzee Karume. Wazee wale waliona hakuna atakayemudu kuongoza nchi.

Mwaka 1980 Mwalimu tena alitaka kuondoka Madarakani na hoja ya kwamba ndiyo kwanza nchi imetoka vitani na Uganda na Mwalimu akiondoka itaonekana kama vile ameiingiza nchi vitani na maswahibu ya vita anataka kumwachia mtu mwingine.

Kwa ivo inawezekana kabisa Mwalimu alitaka kuijenga TANU zaidi kuliko serikali ama aliona mawazo yake na wenzake hayafanani.

Turudi kwenye mada. Kugombana na WB/IMF kwa kushindana nao kanuni ni jambo linaloeleweka, lakini sisi sasa tunagombana nao kwa kushindana nao kwenye kanuni ipi? Hivi sasa sisi ni wajamaa ama ni mabepari?
 
Siyo kweli, maisha kabla ya vita hayakuwa mazuri. Uchumi ambao mwalimu Nyerere aliachiwa na wakoloni mwaka 1962 ulikuwa mzuri. Na uchumi ule ulikuwa mzuri mpaka kufikia Azimio la Arusha. Baada ya Azimio la Arusha uchumi ukaanza kudolola mfululizo, mpaka kufikia miaka ya 1980 ndiyo kikawa kiama kabisa. Vita ya Uganda huwa inatumiwa kama kisingizio tuu cha failed economic policies za mwalimu.
 
Watu hawali principle mzee, watu wanahitaji mahitaji muhimu!
Hayo mambo ya Nyerere kujifanya mwanafalsafa, mwenye misimamo, eti isiyoyumba ilitusaidia nini sisi wakati wa njaa kali?

Ni rahisi sana kuwa na principles kama madhara ya principles zako hayakuathiri wewe au familia yako.
Mwaimu hakuwahi kupigia mswaki mkaa, au kuvaa katambuga, au watoto wake kuvaa midabwada.
Kwa ufupi, hakuwa realistic, and alipenda kufanya majaribio na maisha ya wengine. 😀😀😀
 
Kwa ufupi, hakuwa realistic, and alipenda kufanya majaribio na maisha ya wengine.
Inawezkana alikuwa ni "realistic" lakini akawa na mitazamo isiyo sahihi kwa wakati sahihi.

Ulaya ya Mashariki, Uchina na Urusi huko kote Ujamaa ulishindwa na wala hawakuwa wanaongozwa na Mwalimu. Na Mwalimu inawezekana hakupigia Mswaki Mkaa lakini aliumwa na matatizo ya watu wake. Mwalimu hakufanya makusudi wala majaribio kwa watanzania ila nakubaliana nawe kwamba sera zake za Uchumi zilishindwa kuifanya Tanzania iwe na Uchumi imara endelevu.

Kosa kubwa la wajamaa ni kuchukua mamlaka yote ya kuendesha uchumi na kuyaweka mikononi mwa mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache katika jamii mara nyingi kwenye chama chao cha siasa.

Uchina kuanzia miaka ya 1980 ilianza kuendesha uchumi wa kibepari unaodhibitwa na dola. USSR iliposambaratika nchi zilizokuwa kwenye USSR nazo zilichukua njia ya Ubepari lakini kwa kutumia mifumo ile ile ya kijamaa matokeo yake kama haumo kwenye ngazi za kiuongozi ama kuwa na mahusiano na viongozi wa kisiasa, huwezi kufanikiwa kiuchumi.
 

umenikumbusha mbali..... enzi za RTC kusubiri kikao cha allocation ya radio/baiskeli ili waziuze.
 
Miss, Naona kuna mambo umechanganya.
MR sijachanganya kitu hapo sema tu Bongo mna raha gani? bado sana kwanza joto la hapo ni sababu mme banana sana, vijumba vifupiii, na kuna eneo kuubwa kiluvya, chalinze, bunju, kisarawe nk, mnakunywa maji ya visima, mto Ruvu upo, mto Wame upo hapo karibu. .usafiri shida,makonda wananuka, videm wenu wamechoka,ajili maji ya fungus na typhoid na ikulu mnayo hapo karibu. mawizara yapo hapo. sasa mmehamishia huo uozo Dodoma, wagogo watawatimua wee subiri.
Si afadhali mwende hata hapo Kenya tu mjionee, basi mjifunze, huko kuna afadhali kila kitu poa.

Nyerere aliwasaidia mnalialia ni umaskini, alitaka mtengeneze kitu chenu wenyewe. lkn shida lazima mpitie sasa hivi mngekuwa mbali sana.

Ulaya walimtani kuliko unavyo dhani. yaani iselamagazi umri huu wa miaka 27 baado huuelewi tu, bado
 
NOTHING IS IMPOSSIBLE UNDER THE SUN. WAO WALIWEZAJE SISI TUNASHINDWAJE.

FAILURE IS NOT AN OPTION. MNAWAPA KICHWA SANA. MNAJILEGEZA ,KWA VIJARIBIO KIDOGO ACHA KUPOKEA HATA KUFA KUFA WATAKUHESHIMU.
MSIIGE NIGERIA ETI KWA SABABU WALISHINDWA WAO? NA MIJIFUTA KIBAO UNASALIMU AMRI? KAMA HAMJUI WAO PIA WANATUHITAJI.

KUNA KIONGOZI MHENGA MMOJA HIVI MI NAMPENDA SANA WALIPOMSHINDA NGUVU VITANI AKAJIUA. WAKAIHESHIMU ILE MAHITI MPAKA LEO, MAJUZI TU TUMEKIRUDISHA KICHWA CHETU. KIONGOZI WA GERMANY HITRE, AKAJIFUNZA KWA HUYU MHENGA WEWE JIFUNZE KWA HUYO MHENGA WETU ALIKUWA NA AKILI JAPO HAKUSOMA.
 
Mku kauli mbaya siku zote huwa zinaharibu uhusiano na kumbuka hawa jamaa hawa cha kupoteza na ikiwezeka wanaweza vilevile kuotesha utawala wao na kuweka imaya yao.
Kuna namna ya kula na mtu bila kumshika mkono

Watusaidie kuweka utawala wa Sheria tuko pamoja nao tumechokaisoma no dhidi ya watetezi feki wa wanyonge
 

Huwezi wakwepa ndo uongoza dunia either ushirikiane nao usife au usishirikiane nao ufe.Kila mbabe na mbabe wake alishindwa ticha ndio ataweza huyu akiwa na export ndo ataweza huyu anaetegemeaye kuchukua za machinga na za matrafiki barabarani.Hao sio chadema.
 

Nyerere alicopy na kupaste sera za ujamaa bila kufanya utafiti wa kutosha kuwajua watz waafrica ni watu wa aina gani.Hadi akiondoka nathani alijifunza kitu na kumuona Kambona Bibi Titi walikuwa sahihi juu ya ushauri waliompa aachane na ujamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…