Umasikini unasababishwa na sisi wenyewe tunaowaweka na kuwachekea viongozi wanatuchome nyama wakija kutulaghai. Tunawasganilia kwa ari na nguvu zaidi wao wakila nchi hii kwa kasi zaidi.
Tukiamua hatutakuwa masikini. wewe, mimi, na mwingine na mwingine tuseme wote kwa moyo wa dhati, kwamba basi inatosha na tubadilike sasa.
Tuukatae utawal mbovu, tuukemee uovu wote na matendo yao ya kidhalimu ndipo tutabaki slama.
Sasa hivi hata wale tunaowajua ni wezi wameishaanza kujiandaa kuingia ikulu awamu ijayo, wakituchomea nyama tutawakubali na kuwaruhusu wapanue midomo yao kuendelea kujilambia asali yetu bila huruma.
Tuseme BASI INATOSHA, TUKATE SHAURI ILI TUBAKI SALAMA. Tusiwe kama wabunge wetu sijui wanamuwakilisha nani, utakuta mbunge anaanza kuchangia hoja kwa kushukuru tuliomuweka pale, halafu analalamika toka na kuhuzunika jinsi serikali au waziri fulani anavyotutenda, cha AJABU MWISHO WA YOTE UTASIKIA Naunga hoja kwa asilimia 200, Pumbafu sana hawa..... MUngu awahukumu kwa wanayotutendea.
Sasa wamejigawa kuwa wapo makundi matatu.1= Wabunge wanaofikiri kwa Matumbo, 2= Wabunge wanafikiri kwa vichwa na 3= wabunge wakambi ya upinzani- Hatuponi hata kidogo, tumekwisha kabisa