Umasikini wa kipato unaopelekea umasikini wa kifikra

Umasikini wa kipato unaopelekea umasikini wa kifikra

hitler2006

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2014
Posts
489
Reaction score
454
Huku mtaani si ajabu ukakuta mtu anafurahia kabisa mwenzake kukosa dili fulani, au kufukuzwa kazi maarufu kama kutumbuliwa. Utasikia ooh bora tulingane, na hii imepelekea hata hii inayoitwa "mob justice".

Mob justice haiishii tu kwenye kupiga mtu kisa kaitiwa mwizii, inaenda mbali sana hadi kwenye shutuma za huku uswazi kila mwenye mafanikio utasikia aah "fiiiriiimasooni "yule. Kuna character assasination nyingi sana zinafanyika huku mtaani.

Nyuma ya haya yote ni umasikini wa kipato unaopelekea umasikini wa kifikra.

Si ajabu kukuta msomi kabisaa anashadadiaaa mada kama hizo.
 
Hata ukipigwa ban jf Kuna viumbe wanashangilia. All in all, ukiwa na uwezo, nenda ukaishi sehemu za watu wenye uwezo. Tabu niliyopata nilipofunga dish la DSTV Kimara wakati DSTV ndio inaanza sitakuja kuisahau.

Sikuishia DStv tu, nilifunga full solar na kununua generator kujihakikishia umeme. Kumbuka DStv na solar Ni Kama pembe la ng'ombe, havifichiki.

Maskini wakiwaza nalipa DStv 125,000 taslim hawapati usingizi kabisa. Nilipo Sasa hakuna anayejua Kama Nina DStv au Azam, Kama natumia solar au TANESCO. Kama nimekula kitimoto au sato.
 
Upatikanaji wa pesa mtaani imekuwa ni mgumu sana hivyo mtu ukionekana na gari hizi za kuanzia milion40 kwenda juu watoto wanasoma shule hizi za gharama Kuna asilimia kubwa ya kuchukiwa na jamii iliyokuzunguka kuitwa tapeli ,mwizi au mchawi ni jambo la kawaida kwa watanzania
 
Aisee
Screenshot_20240826_084656_Instagram~2.png
 
Weak Men focus on Other people, Strong Men focus on their Purposes ..

Japo watu wanakera sana ..
 
Back
Top Bottom