Faiza nimepima kwa ajili ya maandalizi ya safari kama mwezi sasa na namshuru mungu nipo salama!!
Ni yote yahusuyo Kujenga penzi!kama nipo sawa!!
Endelea kuwa na wapenzi nje ya ndoa ili upate UKIMWI ama amua ukaoe, mpime wote kabla ya kuoana muisjhi kwa amani na upendo. Nje ya hapo, you are a victim to be.
Wakati mwingine huna budi kuchukua maamuzi magumu hata kama yatakuumiza ila ni kwa manufaa yako ya baadae, asitumie kigezo cha fedha kukudhalilisha, huyo hayuko tayari kuwa na wewe ni vile yawezekana ana kuonea aibu kukupa ukweli wa mambo ila take a brave heart, nawa mikono mtakie kila la kheri nawe ukaa chini ujipange upya.
Duh, kweli nyie mnapendana kikweria kweria.
Mkuu ushauri ni huu, Huyo hafai kabsaaaaaa yaani toka nduki na brake ya kwanza Chamazi., kama unabisha muoe afu upigike utaona unavyokula pilau daily...)
By th way, POLE KWA KULISHWA MIMBWATA.
Ungekuwa mdogo wangu ningekulamba kibao,si kwa sababu nakuchukia ila kwa sababu napenda uzinduke.
Hivi kama ungekuwa na pesa halafu anatoka na mwingine then akakwambia ni kwa sababu ya huwezi majambozi ungekubali? Au ungekuwa na pesa na unaweza majambozi na akakwambia anatoka na mwingine kwa sababu huna mvuto ungekubali?
Au ungekuwa na pesa unaweza majambozi halafu una mvuto ukagundua anatoka na mtu mwingine kwa sababu huwezi kula kwa kutumia kijiko ungekubali?
Kupenda sana kuna mambo yake mazito. Kwa sasa hakuheshimu kwa sababu umemganda wakati unajua anatoka na mwingine,
lakini atakuheshimu pale utakapochukua uamuzi wa kuachana nae! hapo ndio utashangaa sarakasi ya mapenzi ilivyo.Maisha yataendelea halafu itakuja siku utajiona mjinga kwa nini hukuchukua maamuzi mapema.
Nakupa moyo -kumuacha unayempenda ni kazi kwelikweli wengi waliumizwa na hata sasa wapo wanaoumia ingawa hawawezi kufunguka na wamegandana na wanaowaumiza.Hebu achana na huyo binti ili nikuone shujaa
Kwamaelezo yako unaonekana unaupenda sana uking'asti,sasa endelea na kupendwa kwako!!!Naomba mnisaidie japo ushauri!!
Nipo na girlfriend wangu huu ni mwaka wa tatu sasa tokea nasoma mpka hivi sasa naangaika kutafuta kazi, tatizo ni kwamba huyu mwenzangu nimegundua kuwa yupo na mtu mwengine na nilipomuuliza akajibu kuwa ni kweli lkn hakuna wanachofanya na anafanya yote hayo kwasababu mimi simpi chochote ktk mahitaji yake( si mapenzi) na kama nikimtimizia haoni sababu ya kuwa na hao wengine coz ananipenda( na naamini kweli ananipenda na anaonesha hilo)Sasa mwenzenu nipo kwenye mtihani mwanamke wangu namtaka ila roho nayo yaumia!!Naomben ushauri wenu ushauri wa maamuzi magumu!!!!
Naomba mnisaidie japo ushauri!!

huyu ni graduate tunamsubiria kwenye soko la ajira kufanya analytical decisions kweli?
hivi vyuo tunavyosoma sijui hali itakuwaje apo 2020 katika kukabiliana na hali halisi ya dunia ijayo na ya sasa.
et'' nampenda namii najua ananipenda ndo maana ameamua kuwa na mtu amtimizie mahtaji yake kisa mimi sina kazi''' vumilia muoane alafu nawe upate kazi siku moja mkiwa ndani ya ndoa uachishwe kazi gafla ndo utaona segere utavyolicheza bwe...ge wewe.