Umaskini na Nadharia zake

Umaskini na Nadharia zake

Gautten Potten

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1,642
Reaction score
3,426
images (4).jpeg

Tatizo ni Umaskini au tatizo ni kuwapa watu fulani wenye tamaa na njaa Kumiliki wa vitu vyote na kuvifanya kuwa chini Yao na kuwasahau wenzao?

Au tatizo Umaskini ni kitu cha asili na kurithi kama wasemavyo wengine kuwa akiwa baba masikini hadi mtoto anaweza kuwa masikini?

Au masikini upo kimkakati katika uso wa Dunia?
Mana Kuna wale wanasema Dunia haiendeshwi na watu Bali mfumo Mana hata ukiondoka wewe akaja mwingine atakutana na pattern Kisha kuendeleza na kuunda taasisi Kama ilivyokuwa awali.

Au Umaskini ni kitu umepangiwa na Mungu tangu kuumbwa hadi kuzaliwa?

Kama tunaangamia kwa kukosa maarifa, vipi wanaouza maarifa hayo kwa gharama kubwa?

Maarifa, Kazi na Pesa vimeshonwa kwa Pamoja ktk ulimwengu huu wa sasa, je maskini atapaje maarifa akiwa hasa pesa na hana kazi?
Achague kipi aache kipi ?

Weka Nadharia ambayo unafikiri inaweza kuwa mlango wa umasikini kwa vijana na wazee walio wengi, unaweza saidia mtu kuamsha UFAHAMU wake.

Huwezi jua andiko lako linaweza Ponya wangapi wenye kuzingatia.
 
Kaza mpaka mwisho usikubali kulazimishwa kuwa masikini kwa namna yoyote ile.
Pambana na Madalali.
 
Back
Top Bottom