Umaskini ukikomaa huzaa ushirikina

Umaskini ukikomaa huzaa ushirikina

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
PENYE UMASKINI NDIPO UTASIKIA MITIZAMO MINGI YA KISHIRIKINA.

Kuna sababu nyingi za watu kuwa washirikina na kati ya sababu hizo umaskini ni moja wapo.

Umaskini wa mawazo na kifedha ni sababu kubwa sana nyuma ya washirikina.

Kwenye umaskini ndio utasikia wengi wakianguka mapepo, kulalamika wameibiwa nyota na matukio mengi ya kutafuta utajiri kupitia damu za watu.

Umaskini ukikomaa humfanya mtu aamini kuwa hakuna utajiri wa juhudi bali atamuona kila tajiri ni mshirikina hivyo naye ataanza kutafuta huo ushirikina ili awe tajiri.

Maskini hata ugonjwa wa kawaida kwake ataona karogwa, matokeo ya uzembe wake ataona kama kuna mtu kamuibia nyota yaani akili yake muda mwingi inakuwa inafikiria tu ushirikina.

Jaribu kuwasikiliza wazee zaidi ya watano maskini nina uhakika wengi wao watahusisha umaskini wao na ushirikina kama hawatakwambia wamerogwa basi watakwambia utajiri ni dhambi.

Umaskini ni janga lingine kubwa sana ambapo kama wapambanaji tulione kama tatizo la msingi kuliondoa hata watoto wetu waanzie kwenye hatua moja mbele.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
fikia ndoto zako.
 
Ni kweli kufanikiwa kunahitaji ushirikina, lazima ushirikiane na watu vizuri ili ufanikiwe .
 
fikia ndoto zako
 
Masikini yeyote akikuona una biashara zako na zinaenda vizuri atakuambia, wewe lazima umeenda kwa mganga
Umasikini ni LAANA
 
PENYE UMASKINI NDIPO UTASIKIA MITIZAMO MINGI YA KISHIRIKINA.

Kuna sababu nyingi za watu kuwa washirikina na kati ya sababu hizo umaskini ni moja wapo.

Umaskini wa mawazo na kifedha ni sababu kubwa sana nyuma ya washirikina.

Kwenye umaskini ndio utasikia wengi wakianguka mapepo, kulalamika wameibiwa nyota na matukio mengi ya kutafuta utajiri kupitia damu za watu.

Umaskini ukikomaa humfanya mtu aamini kuwa hakuna utajiri wa juhudi bali atamuona kila tajiri ni mshirikina hivyo naye ataanza kutafuta huo ushirikina ili awe tajiri.

Maskini hata ugonjwa wa kawaida kwake ataona karogwa, matokeo ya uzembe wake ataona kama kuna mtu kamuibia nyota yaani akili yake muda mwingi inakuwa inafikiria tu ushirikina.

Jaribu kuwasikiliza wazee zaidi ya watano maskini nina uhakika wengi wao watahusisha umaskini wao na ushirikina kama hawatakwambia wamerogwa basi watakwambia utajiri ni dhambi.

Umaskini ni janga lingine kubwa sana ambapo kama wapambanaji tulione kama tatizo la msingi kuliondoa hata watoto wetu waanzie kwenye hatua moja mbele.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
fikia ndoto zako.
Iko wazi kama ya kichaa.
 
Maskini wengi wanaamini waliofanikiwa ni mafreemason
 
Back
Top Bottom