flyingcrane
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 241
- 88
Alshabaab ni kundi lilopata umaarufu sana Afrika Mashariki hasa Kenya. Kundi hili limestawi kwa kuajiri vijana wengi kwa siri kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania. Nakumbuka kuanzia mwaka wa 2009 wakati vijana wengi wa mitaa ya Mombasa hasa majengo ninayokaa mimi walivyokuwa wakipiga gumzo kuhusu kundi hili la kivita lililokuwa likiajiri na kulipa vijana 120,000ksh. Waliopewa kandarasi walikuwa masheikh na mambo haya yalikuwa si yasiri. wengi waliacha shule na kujiunga, waliomaliza shule pia walijiunga. Askari polisi hawakulitilia maanani jambo hili sababu kenya haikushambuliwa na magaidi wala hatukuwa kwa vita nao. Pindi alshabab walipoanza mashambulizi na kuteka nyara ndipo serikali iliposhtuka lakini tayari kitumbua kilikuwa kimeingia mchanga. kama vijana wetu wangekuwa na ajira, elimu ya kutosha na viwango vya umaskini vingekuwa chini hatungekuwa na hii shida nchini.. Hivi sasa KDF inauwa vijana wetu wa Kenya, watanzania na baadhi ya waganda waliokwisha vuka mipaka kwenda somalia. vita hivi ni vya ki akili tunauwana wenyewe kwa wenyewe. Alshabaab ni jina tu lililotuchangana