Umedanganya wangapi?

Umedanganya wangapi?

Jewel

Senior Member
Joined
May 1, 2008
Posts
180
Reaction score
65
KUNA mdau kanitumia hii, isome, ni kweli?
Mapenzi ni kitu kisichodumu kwa muda mrefu (do not last longer or is something temporary).
Ni kwa sababu ya mapenzi (?) leo upo na uliyenaye na unajihisi ndiyo umefika.
Huenda baada ya muda utaachana na huyo na baada ya muda fulani utapata mwingine na utamsahau kabisa huyu uliyenaye sasa ambaye unahisi bila yeye dunia haikaliki.

Kuwa mweli katika nafsi yako, jiulize, tangu ulipoanza kuchakachua miaka ileeeh, ni wangapi umewaambia unawapenda kwa dhati lakini sasa haupo nao?
Umewadanganya wangapi kwa kuwatamkia maneno kama vile honey, sweetie, my love, baby, mahabuba, ma shababi, la aziz , nikinywa maji nakuona, sipati usingizi bila wewe, ukiniacha nitajiua n.k lakini leo yako wapi?

Kwa mtazamo wangu, mapenzi ni kama siasa (politics) zinazokaribiana na ukweli.
Licha ya kwamba binadamu anahitaji kupenda na kupendwa tusijisahau.

 
hii ni tabia tu ya mtu sikweli kwamba wengi wako hivyo. ukizoea kunywa pombe utahitaji unywe nyingi zaidi na iana nyingi zaidi
 
sijawahi kudanganya.... mie uongo kwangu mwiko

nilipokuwa na ex nilikuwa na hisia juu yake, nilimpenda penzi lilipochuja na kuisha nilimwambia ukweli sikufeel kama mwanzo kila mtu akatafuta ustaarabu wake, kwa hiyo hakuna uongo hapoo..........
.
 
true...mapenzi siku hizi isanii tuu..maneno matamu kunogesha story tuu
 
Kudanganyaaa...hapana! Ujue hakuna anaeweza ku-predict future,so kila mtu anapoingia kwenye mahusiano anakuwa na expectations kwamba mahusiano aliyopo atafika nayo mbali....lakini mambo yakiharinika katikati ya safari haina budi kuisitisha safari hiyo. Sasa hiyo haimaanishi...kwakuwa nilimwambia nampenda sana hapo mwanzo then nilikuwa muongo au nilimuita sweet names halafu sikuwa real....Hapo nakataa!!
 
hakuna kudanganyana,wala kuchokana,ni tabia na hulka ya mtu binafsi kudanganya mtu tu.hasa hasa wale wasio na misimamo katika mapenz,lakin wenye misimamo hawadangany wanateleza tu.
 
mie nimedanganya labda kwa uchache marcopolo 3 zikiwa nyomi.
 
mazingira nayo yanasababisha watu waachane, haimaanishi unapomuacha mtu ulikuwa humpendi/unamdanganya..
 
mazingira nayo yanasababisha watu waachane, haimaanishi unapomuacha mtu ulikuwa humpendi/unamdanganya..

Husn ! Moja ya vinavyofanya nikukubali ni comnt kama hii ! Short & clear imejitosheleza, utamaliza kura zangu!
 
sidhani kama nilidanganya coz wote kwa kipindi nilichokuwa nao nilijiona nimefika na nilitegemea kuwa nao maishani but shit happens unajikuta umetosana naye na kuhamia kwa mwengine ukiwa na expectation zile zile......
 
Nashkuru sijawahi kudanganya, nikikutongoza basi hakyanani nitakuoa.
 
bichwa limevimba, una hela ya kunipeleka india kwa matibabu? Lol.

Si lazima kusubiria hadi bichwa livimbe, niko Congo Drc kwa sasa, namalizia kazi nikirudi tu Tz jiandaet kupelekwa kwa "odinary medical check up" Apollo hosp
 
Back
Top Bottom