Umefika muda sekta ya Vicoba kutungiwa sheria rasmi na chombo maalum cha kuwasimamia

Fahami Matsawili

Senior Member
Joined
Mar 8, 2018
Posts
172
Reaction score
153
Umefika muda sekta ya Vicoba itungiwe sheria ya kuwasimamia na kupewa chombo maalum cha kuwa mwangalizi wao kuliko ilivyo sasa haijulikani wapo wizara gani kati ya wizara ya fedha na mipango au wizara ya viwanda Biashara na Uwekezaji...

Kwa sasa Wananchi milioni 5 wamejiunga kwenye Vicoba kwa nia ya kujipatia kipato hadi Leo vikundi vya Vicoba nchi Nzima vina Mtaji Trillion 1.4

Fedha hizi ni nyingi sana hasa kwenye uelekeo wa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu John Magufuli ya Ujenzi wa Sekta ya Viwanda kuelekea uchumi wa kati 2025...

Badala ya Vicoba kuwa kwenye mfumo wa kuweka akiba na kukopa tuu sasa ni wakati wa Vicoba kutumia fedha hizi katika kuwekeza kwenye Viwanda na Miradi mikubwa ambayo mtazalisha ajira zaidi na mtapata faida zaidi ya miradi yenu mtakayooanzisha....

Tumeona hayo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii imetoka kwenye mfumo wa kuweka akiba tu hadi pension na sasa mifuko imeanza uwekezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi...

Sasa muda wa kuwa na sheria na chombo Maalum cha kuwalea na kuwasaidia nadhani Umefika lakini zaidi nimefurahi zaidi kuona vijana wa bodaboda na bajaji wameanza kuitikia mfumo huu wa Vicoba kwa kujiunga pamoja na kuchangishana na kuweka akiba nimepita kwenye banda lao wamenambia wengine wamenunua bajaji zao kutoka bajaji za mikopo kupitia mfumo huu wa Vicoba......

Tuna Vijana wengi wapo kwenye sekta ya bodaboda na bajaji karibu vijana milioni 2 wamejiajili huko na wengine wanaendesha maisha maisha yao, wamejenga na wengine wanalipa kodi kupitia bajaji na bodaboda.....

Kazi ya Mamlaka husika ni kuwasaidia hawa vijana wenzangu kuondoa changamoto zinazowakabili kama Elimu ya usalama barabarani ya Mara kwa Mara wawe na Vazi rasmi lenye no na kituo Maalum kama wenzenu wa nchi ya Rwanda.

Polisi wawe rafiki na bodaboda na bajaji katika kuwasaidia badala ya kuwachukulia kama wahalifu na wahuni.

Vijana wa Bodaboda na bajaji milioni 2 tulionao sasa kama kila mmoja anakusanya wastani wa Elfu 10 kila Mmoja kwa siku ina maana sekta ya bodaboda na bajaji kwa siku nchi Nzima wanaingiza Shillingi billioni 20 kwa siku..

Ina maana hawa wakisaidiwa kupewa Elimu ya kujiunga na kujiwekea akiba kiasi kidogo tu kutoka kwenye hiyo Elfu 10 wanayopata kila siku kama hawa wenzao ambao tayari wameanza tutakuwa na vijana wenye vipato vizuri na watawekeza kwenye miradi mikubwa ya Uzalishaji wa kiuchumi..
 
Maana hao mafisi wa serikalini watakapopewa mamlaka ya kuundia sheria na kanuni jua wazi wataanza kuunda mifumo ya udokozi na mbaya zaidi watatafuta mianya ya kufilisi.....
 
VICOBA vimechukua mwanya na udhaifu wa mabenki wa kutokuwa na huduma za kuwafikia wanyonge, sasa hivi mabenki yanainyemelea hiyo steki nono ya VICOBA bila hata aibu, serikali itunge tu miongozo lakini isiwaingilie kwenye mipango yao, wakitaka kuweka na kukopa sawa, wakitaka kuwekeza kwenye viwanda sawa...yawe matakwa yao.
 
Mimi nadhani Wa endelee kuwa huru no need of government regulation.Kwa sababu ukisha ingiza serikali kwenye ishu kama hizi tutarudi kulekule kama mifuko ya pension ilivyofanywa.
 
Kwani utaratibu uliopo unashida gani...!?
Serikali ikitia mguu tu, vicoba vitaanza kuugua na kufa...
 
Nafikiri kuna mkono wa serikali katika suala hili ndo mana wanatakiwa wajisajili wizara ya mambo ya ndani.. lakini wamepewa uhuru wa kujitawala.. Sekta huru hufanya kazi kwa uhuru sana.. ukawii kusikia mambo ya kama ya mifuko ya kijamiii...
 
Bora ibakie hivyo hivyo, wawe huru kufanya mambo yao kutokana na utaratib7 wao, kwani hata hivyo wanajiendesha vyema, ndio maana husikii kelele wala malalamiko ,

Lakini pakianza kuwa na mfumo mwongine sijui wa kusimamia jii kitu basi ni dhahiri kabisa hapo ni mwanya wa ulagi wa pesa za wanachama tu na sio tena kwa lengo la kuwanugaisha kama walivyo panga,

Sasa hivi mwanachama wa vicoba , anaweza kupata mkopo muda wowote bila vipingamizi , lakini eti ikianza sijui tume au nini cha kusimamia basi hapo utaona malalamiko yataanza tu kwa wanachama kunyimwa mkopo kwa muda unaostahili ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…