Umeitwa kwenye hii kesi,ungesuluhisha au kushauri vipi?


Unajuwa dadaangu hakuna kitu kibaya kama kudharauliwa na wifi yako alifanya hayo kwa mumewe. Dharau hasa ikitoka kwa mwanamke ina sumu kubwa kwa ndowa na huyo mdogo wako aliila hiyo sumu muda mrefu kiasi cha kuuwa kabisa penzi lake. Kifacho kinatabu kuja juu.

Iwapo mambo yaliyomfanya aowe hakuyapata kwa wifi yako na badala yake anayapata pengine, shida ya nini? Huyo wifi yako akashughulikie alichokithamini na akiondoka basi ndugu yako atahalalisha yule anaemjali.
 

Loose ends hapo ni kwamba huyo jamaa anajificha kwa alibi kwamba isingekuwa mke kuwa busy hivyo asingeenda kwa h/girl..
 
Pamoja na kuwa wote wanamakosa Lakini Pia Hakuna mapenzi ya Kweli kati yao

Ushauri; Wote watubu Kwa Mungu wao kwa makosa yao na Kisha wao wasameheane na Kuanza Upya

Wakirekebisha kila walipo kosea

Bila Mungu Hawataweza, Ni Lazima kuombe Neema ya Mungu
 
Pamoja na kuwa wote wana makosa lakini haimpi haki mwanaume kutembea na housegirl....... Yaani wanawake wote mpaka atembee na hg? Na mnapoambiwa ndoa inahitaji uvumilivu na ukomavu ndio hapo sasa........ Kama mwanaume angetafuta njia mbadala ya kumaliza tatizo na mkewe....... Si ndo maana mnajiita nyie ni kichwa cha familia? Kichwa kikiamua maamuzi 'utumbo' itakuwaje?


Kitendo cha mke kurudi saa sita usiku tu inaonyesha kuwa ndoa yao ina walakini,

keti nao wakueleze vizuri kuna kitu ambacho hakipo wazi hapo....na hakuna wateja wa saa sita usiku............

Nimachokiona ni kama wanakomoana, ndoa haina kukomoana, ndoa haina mbabe, ndoa inabebwa na kusikilizana, kujitoa, na KUVUMILIANA.......

Hawana watoto hao wana ndoa? Na kipindi mke kajifungua huyo mwanaume alikuwa anatembea na nani? Maana kipindi kile ni cha kusubiri kati ya wiki 2-siku40 au zaidi kutegemea na mwanamke na mwanamke......je huyo mwanaume alimaliza vipo mihemko yake?


Kuna tatizo kwenye hiyo ndoa, na tatizo si la mke kuchelewa kurudi wa lamume kutembea na hg, nahisi kuna kitu hawajakisema....


 
matatizo mengine wanawake tunachangia sisi wenyewe, hasa kuwepo kwa nyumba ndogo. wewe una mume, huna haya mtoto wa kike J3 mpaka j2 kwako unarudi 5 au 6 usiku. hujui watoto wameshindaje, wanaumwa, wamekwenda shule, wana homework. wewe ni pesa, pesa na wewe. hujui mume kala nini, kapenda chakula, basi umeshindwa vyote, na kitu tamu ambayo ni haki yake huwezi kumpa! salon gani hiyo ya kurudi ma-usiku kila siku, huyo atakua ana ki serengeti somewhere kinamkuna, ndio maana haraka haraka kakimbilia anataka kuachika, maana alikua anaisubiri hiyo siku kwa hamu. wifi yako hajatulia. shindwa vyote kwa mumeo, lakini unyumba MUST, anataka aende wapi? sasa kamkomoa, kachukua hsegal, ya nini aende mbali na anayemhudumia yeye na watoto wake yuko humo humo ndani. aache kulalama na kusema eti yuko kwenye siku zake, huo ni uzushi. kuna njia kibao za kumridhisha mwenzio hata kama uko kwenye siku. kanogewa kwa kiserengeti chake aache kutunga hadithi za vitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…