Umejifunza nini kupitia kwa Louis Suarez?

The Icebreaker

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
22,278
Reaction score
65,817
Mchezaji wa soka Louis Suarez raia wa Uruguay aliyekua akiichezea Club ya Barcelona ya Spain toka mwaka 2014 - 2020 akitokea Liverpool,aliambiwa na kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman kua alikua na uwezo mdogo wa kucheza soka la ushindani na umri wake umeenda hivyo hakua kwenye mipango ya kocha na akaambiwa atafute team nyingine,

Suarez akapata nafasi ya kuichezea Atletico Madrid ya Spain msimu wa 2020-2021 na kuisaidia Atletico kushinda kombe la La liga kwa kufunga magoli 21 assist 3 katika mechi 32 alizo cheza,Suarez alifunga goli la ushindi dhidi ya Real Valladolid na kuipa Atletico kombe la La liga kwenye mechi ya mwisho ya ligi ya Spain huku Barcelona team iliyomkataa akimaliza ligi kwa kushika nafasi ya 3

Baada ya kushinda kombe la La liga,Suarez alisema;

"Barcelona hawakunithamini,waliniona mtu mwenye uwezo mdogo na Atletico wakanifungulia milango na kunipa nafasi,
Siku zote nitaishukuru hii club kwa kuniamini"

Je, wewe umewahi kua rejected sehemu yeyote kisha ukatusua sehemu nyingine?

Mods msihamishe hii mada coz sio tu ni ya Sports bali pia ina funzo kwenye maisha nje ya Soka.



 
Kesho Kigwangalla nae ataanza kujilizaliza na kujiita Luis Suarez "Ooh kilichoniumiza zaidi Jamhuri haikuni thamini, iliniona sifai na watu wakaniita fisadi".

Barca daima hawana fadhila kwa wachezaji wake, kumbuka alichofanywa Samuel Etoo na Ronaldinho kipindi wapo kwenye form balaa.
 
Ok, ila bado wana kazi ya kufanya unaweza kuwa wa kwanza kwenye darasa la wajinga.

Ni ubovu wa madrid na barca ndio umewarahisishia kuchukua ubingwa. Hao wangekuwa kwenye kiwango chso basi nao ilitakiwa wawe bora sana kubeba ndoo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Huyu hapa
 

Huyo gaucho mtoe hapo, pumzi ilikata mapema.. ..huwa nashangaa baadhi ya mashabiki wanamtukuza gaucho wakati hakua na msaada wowote katika timu.

Kwanza huyo kocha tungemuona mpumbavu na asiefaa kuinoa Barca endapo asingechukua maamuzi ya haraka kumtimua gaucho pale Barcelona.


Hongera sana raisi wa barca na kocha wa wakati huo kwa uamuzi mulioutoa wa kutimua, otherwise mngebaki mnalialia tu, bila shaka hata UEFA isingeshiriki kwa uwepo wao.



πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Katika players walioondolewa pale barca huyu mshkaji kaniumiza sana pamoja na Semedo.



πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Kwa Semedo hapo naungana na wewe; ila Suarez ni bahati ndo imembeba ila hana hadhi ya kuichezea Barca...alikua kama Kun Aguero au Tamy Abraham.

Mkuu unamkosea sana Suarez.. ..ebu fuatilia nani goalscorer pale baada ya Messi nani kama sio suarez! Huyo griezmann kafeli, mfumo wa pale umemkataa.

Kwa Aguero bado yuko on πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯ sema kocha hakua anamchezesha mara kwa mara, sijajua wana bifu gani nae! I'm so happy akacheze barca, hope mfumo wa pale atauweza tena vizuri.




πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
umeandika nini Sasa kwani huyu gaucho na etoo hawajahi kutwaa ndoo hapo camp nou?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…