Umeme kukatika ifikika jioni

Umeme kukatika ifikika jioni

lui03152

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2020
Posts
266
Reaction score
377
Nimekuwa nikipata changamoto hii kwa muda sasa kila inapofika jioni taa zinapowashwa umeme umekuwa una kata na kuzima mara kwa mara. Na baadhi ya vifaa kama vile AC kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya umeme kukosa nguvu wakati mwengine baadhi ya taa kufifia mwanga.

Lakini cha kushangaza wakati hali hii inapotokea huwa kwenye remote control ya mita huwa inaandika LOW VOLTAGE, kingine wakaginwa hali hii pia nimejaribu kuangalia nyumba za majirani hazikumbwi na hali hii zenyewe huwa umeme unawaka tu.

Lakini nimeuliza baadhinya mafundi wanasema inawezekana mahitaji ya umeme yameongezeka sana kuliko uwezo wa transforma katika eneo letu. Bado sijatoa taarifa tanesco kuhusiana na changamoto hii. Naomba kufaham kama kuna yeyote mwenye uzoefu na hili anijuze ili hata kama nitatoa taarifa tanesco niwe na rejea ya kutosha.

Natanguliza shukrani, na kiambatisho cha picha ya display ya remote ya luku ikionyesha inavyosoma wakati wa hali inapotokea.

20240530_202738.jpg
 
Back
Top Bottom