A
Anonymous
Guest
Kwa nini kila kukiwa na Mechi za Simba, Yanga au Azam umeme unakatwa Meatu?
Kumekuwa na changamoto ya kukatika kwa umeme bila mpangilio wala utaratibu maalumu Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Hali hii imekuwa kero kubwa kwetu wakazi wa Wilaya ya Meatu kwani hakuna taarifa yoyote ya utaratibu wa ukatwaji wa umeme wala tamko la kurejea kwa mgao tena kwani ilitangazwa kuwa mgao wa umeme umesitishwa ila kwa nini Meau bado tunateswa na mgao?
Kero hii huzidi zaidi kunapokuwepo Mechi kubwa za mpira wa miguu hapa nchini, kama Mechi za Simba, Yanga au Azam. Umeme hukatika muda mfupi kabla ya mechi, hadi tunajiuliza, au kuna biashara gani kati ya TANESCO na hizi kumbi za kuonesha mpira almaarufu kama vibanda umiza?
Tunaomba suala hili litatuliwe, ili nasi wananchi wa Meatu tufurahie uwepo wa nishati ya umeme kwenye kuendesha shughuli zetu za kijamii zinazohitaji nishati ya umeme bila kukatiwa katiwa ovyo, na iwapo kuna tatizo basi tupewe taarifa ili tuweze kujipanga kwa hilo.