Elections 2010 Umeme na anguko kubwa la chama cha magamba (ccm)

Elections 2010 Umeme na anguko kubwa la chama cha magamba (ccm)

Kajuni

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Posts
483
Reaction score
186
Naandika nikiwa na furaha!!!! kivipi? kwani hakika anguko kubwa la chama cha Magamba limekaribia sitaki kuwa shehe Yahaya (the late RIP) lakini ni mambo yanayo onekana kwa uwazi kabisa (Black and white). Na hakika hayaitaji mtabiri kuyaona. Vijana wana hari kubwa sana kuleta mabadiliko.
Kilichonipa furaha ni kelele pindi umeme unapo katika hapa mtaani kwangu...mayowe na nderemo usikika vijana wakisema. TUMPIGE CHINI RAISI kwani kazi imemshinda na haya sio maisha bora kwa mtanzania. Kijiwe kimejaa vinyozi, wauza samaki, wauza nyama etc ambao vipato vyao viko hatarini kwa hili tatizo la mgao. Takwimu zina sema ni asilimia 14% tu ndo chama cha magamba kinawafikia kwa huu umeme wa mgao.... what a shame!!!! 50 YRS baada ya uhuru.

Jamani wakati umefika kukaza uzi... tena nafikiri hizi ishu za bajeti zinaweza kuwa ngumu kueleweka. Lakini hili la umeme watu wanalielewa fika. Visingizio vimekwisha kwani mvua zimenyesha na mitambo yote imewashwa lakini mgao upo pale pale tena ndo umeongezeka maradufu. Wala tusiumize kichwa na matendo ya binti Kiroboto mjengoni na mengine mengi kama hayo.

Haya shime wakati ndo huu tuchukue hatua... napenda kuwakilisha.
 
una hoja ya msingi sana kuhusu hili tatizo la umeme, ni kweli kabisa miaka 50 c mcheza lkn bado umeme tatizo na huku tuna vyanzo kibao vya umeme kama; maji, gesi, makaa ya mawe na upepo.
vema sana ila kijana lugha kidogo inakupiga chenga mf hari badala ya ari, usikika badala ya husikika
 
Umesahau chanzo cha jua. Chad, nchi maskini zaidi duniani, ina taa za barabarani mji wote wa N'djamena, kwa sababu ya nishati ya jua! Sijui Dar ina taa za barabarani vile??¨!!!!
 
Nafikiri jamaa wameshindwa kusoma alama za nyakati,itakula kwao hivi karibuni!!
 
Back
Top Bottom