KERO Umeme umekuwa shida kubwa Rufiji. Kwa siku umeme unakata hata mara 30

KERO Umeme umekuwa shida kubwa Rufiji. Kwa siku umeme unakata hata mara 30

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Buzi Nene

Senior Member
Joined
Feb 10, 2020
Posts
148
Reaction score
340
Huku wilaya ya Rufiji umeme unakatika sana sana,kwa siku umeme unakatika zaidi ya mara 30 ,sio uongo ni kweli kabisa,wanaoishi huku ni mashahidi

Mimi ninaisha Nyamwage hapa lakini hii imekuwa kero sana, hii shida imeanza muda mrefu ila kwa kipindi cha mwezi wa tatu na huu wa nne imezidi maradufu.

Staili ya kukatika kwa umeme ni unakatika baada ya kama dakika 10 au 20 unarudi
Staili nyingine ni kama unakatika kama radi tena unakatika sekunde mbili unarudi hii ndio mara nyingi zaidi.

Najua huu sio mgao wa umeme, inawezekana kuna changamoto kwenye njia za usafirishaji wa umeme.

Tunaomba TANESCO watusaidie katika hili sisi wananchi tunateseka sana

Buzi Nene.
 
Poleni mno ila kinachonisumbua na kutozielewa Mada kama hizi why umekuja kulalama humu wakati tatizo lipo hapo na jawabu lipo hapo hapo,why usifanye service protest hapo kwenye ofisi za Tanesco?,make sure GM hapo haondoki ofisini mpaka ametoa majibu mwafaka au choma moto hiyo ofisi na Tanesco nchi nzima watahamia hapo,ni wakati wa kuongea lugha watakayoisikia na sio kulalama humu,push back
 
Na hili si kwa Rufiji Tu, hata hapa Mtwara MC utaratibu ndiyo huo huo. Style ya ukataji wa umeme si rafiki kabisa unaweza kuunguza vifaa vya umeme.
 
Nashukuru sana Moderator kwa kurejesha uzi wangu
 
Rufiji na mafuriko hayo umeme lazima uzingue

Ova
 
Nitoe shukran za dhati kwa uongozi wa jamii forum kutusaidia sisi wananchi wa Rufiji kupaza sauti
 
Ila hali bado ni tete,tangu asubuhi umeme umekatika zaidi ya mara sita,na mpaka muda huu naandika posti hii 15:10 Umeme hakuna umekatika mida saa nne au saa tano
 
Nashukuru uzi ulirudishwa jana usiku baada ya kutoa malalamiko yangu,pia nimefurahi habari pia imerushwa Whatsapp kwenye channel ya Jamii forum
Hongera Sana. Natumai watalishughulikia hili
 
Back
Top Bottom