DOKEZO Umeme wa REA vijiji vya kata za Kagoma wilayani Muleba usitolewe kwa ubaguzi

DOKEZO Umeme wa REA vijiji vya kata za Kagoma wilayani Muleba usitolewe kwa ubaguzi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ni miaka takribani sita tangu mradi wa umeme kwenye baadhi ya vijiji vya kata za Kagoma wilayani Muleba upite lakini wananchi walio wengi mpaka sasa hawajaunganishiwa umeme. Vijiji vilivyoathirika zaidi ni kijiji cha Manyora, Katwelelo na Muyenje.

Kijiji cha muyenje kiliathirika zaidi kwa sababu kipindi mradi huu unafanyika kwenye hivyo vijiji, mwenyekiti wa kijiji alikuwa ni mpinzani wa CCM (alikuwa ni CHADEMA) na taarifa za ndani ndani inasemekana walikataa makusudi kufunga huo umeme ili kuwakomoa wananchi walioichagua CHADEMA badala ya CCM.

Mbaya zaidi ili kuziba huu uovu wao, walikua wanafunga umeme kwenye baadhi ya nyumba chache tuu ili kuwaaminisha wananchi na waliofungiwa umeme huo ni wana CCM kindakindaki au watu mashuhuri kwenye kijiji. Wananchi wamefuatilia mara kadhaa, wameandikisha majina ya wanaohitaji kufungiwa umeme lakini mpaka leo hamna kitu.
 
Back
Top Bottom