Umeme wakatika Dar na Zanzibar, TANESCO yasema utarudi saa 5 asubuhi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaskitika kuwatangazia wateja wake, kuwa kumetokea hitilafu kwenye kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Ubungo leo Desemba 15, 2021 saa 3:18 asubuhi.

Mafundi wanaendelea na jitihada za kutatua tatizo hilo, kufikia saa 5:00 asubuhi huduma ya umeme itakuwa imerejea maeneo yote.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza .
IMETOLEWA NA;
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Hapa Kibamba Dar es salaam umerejea dakika kama 2 zilizopita.
 
Hadi sasa Tabata umeme haujarudi. Hizi ni hujuma.
 
Miaka 60 ya Uhuru umeme bado unakatika tena kwenye miji mikubwa!!!?

Kwa staili hii somo la Uzalendo haliwezi kueleweka.
 
Kwa jina la muungano wa Tanzania umeme rudi Zanzibar!
 
Mh hi inchi sijui Nani katuroga wallai ...yaan kuna nchi ndogo hapa jirani tu umeme haukatiki ovyo ovyo kabisaaaa na Wala hawana vyanzo vingi vya kufua umeme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…