Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Ni chakula kizuri sana kutumia kama kifungua kinywa (breakfast) cha mtoto kwa sababu kina kiasi kikubwa sana cha virutubisho.
Chakula hiki kitamfanya mtoto wako awe na siku nzuri yenye uchangamfu. Chakula hiki pia ni kizuri sana kama una shughuli nyingi, kwani utakiandaa kwa muda mchache tu.
Chakula: Rojo la karoti na nanasi
Uuda wa kuandaa: Takribani dakika 20
Umri: Kuanzia miezi nane
Katika kuandaa chakula hiki utahitaji
½ kikombe cha vipande vya nanasi,
Karoti moja ambayo umeikata vizuri na
Mdalasini.
Namna ya kuandaa
> Anza kwa kuchanganya vipande vya karoti na nanasi katika chombo kimoja kisha upike mchanganyiko wako kwa muda wa dakika 7 – 10 au mpaka utakaporidhikia na ulaini.
> Baada ya kupoa hamishia kila kitu kwenye blenda na usage mpaka utakapopata wepesi sahihi kwa mtoto wako. Kama mtoto wako amefikia miezi 10 unaweza kuponda badala ya kutumia blenda.
> Unaweza kutumia maji au maziwa katika kudhibiti wepesi wakati wa kusaga au kuponda.
> Malizia kwa kuongeza kiungo ambacho mtoto wako anakipenda, mimi nimetumia mdalasini.
> Wewe unaweza kutumia kiungo ambacho kinampendeza mtoto.
Unaweza kutunza chakula hiki kwenye friji na kumpa mtoto kidogo kidogo.