SoC03 Umenifundisha kufundisha

SoC03 Umenifundisha kufundisha

Stories of Change - 2023 Competition

Christology

New Member
Joined
Jun 5, 2023
Posts
2
Reaction score
2
UMENIFUNDISHA KUFUNDISHA
Jumatatu moja tulivu, wanafunzi wa darasa la tano waliingia darasani baada ya kutoka Paredi. Mwalimu mgeni machoni mwao akaingia darasani. Wanafunzi wote wakasimama na kusalimia kama ada yao. Mwalimu akaitikia na kuwaruhusu wakae. Akaenda ubaoni na kuandika jina lake.

“Naitwa Madam Elizabeth. Nitakuwa na nyinyi kwa kipindi chote nikiwafundisha masomo ya lugha.” Mwalimu akajitambulisha na kwenda kukaa kwenye kiti chake akipitia baadhi ya mafaili aliyofika nayo. Utulivu mkubwa ukawepo darasani hapo, hali iliyomfanya mwalimu huyo afurahi.

“Nimetokea kuwapenda sana, mimi napenda watoto watulivu na wasikivu.” Akanena hayo na kuwatazama wanafunzi wake kwa zamu. Ghafla akamuona mtoto mmoja mchafu wa mavazi hadi vitendea kazi vyake. Kilichomchukiza, mtoto huyo alikuwa anasinzia. Akamrushia chaki na kumshtua kutoka kwenye usingizi nyemelezi.

“Unaitwa nani?” Mwalimu akauliza kwa sauti isiyo na mzaha.
“Naitwa Iddi Mbonde.” akajibu huku akifikicha macho yake yaliyoendelea kumsaliti. Sare zake za shule zilifubazwa na uchafu. Hakufunga mkanda, bali kamba ya mkonge na kuzidi kumchefua mwalimu huyo.
“Kaa chini.” akafoka, na mtoto huyo akatii.

Muda huo ulikuwa ni wa kipindi cha Hesabati, mwalimu wa zamu alipoingia, mwalimu mpya akapisha na kwenda ofisini.

Japo alisema anawapenda wanafunzi wote, ila moyo wake ukatokea kumchukia Iddi. Jina lake liliganda kichwani.

Kwa kipindi chote cha muhula wa kwanza na wapili. Mwalimu Elizabeth na Iddi hazikuwahi kuiva. Hata kwenye adhabu, Iddi aliadhibiwa zaidi.

Chuki ya Mwalimu kwa Iddi iliongezeka kila alipofeli somo lake. Naye Iddi akamwogopa mwalimu, alikosa raha kila amuonapo darasani au mahala popote.

Mwisho wa muhula, walimu walitakiwa kuwajazia watoto ripoti zao. Na hapo kulikuwa na kipengele cha kuorodhesha tabia za watoto na uwajibikaji wao darasani.

Alipoifikia ripoti ya Iddi, aliona jinsi masomo mengine alivyofaulu. Ila somo lake alianguka. Hii ilimfanya pale kwenye kujaza tabia za wanafunzi, ampe alama F. akiwa na maana haikumpendeza hata kidogo.

Wakati anaiweka karatasi hiyo kwenye file la Iddi, ndipo alipotamani kujua mtoto huyo alipokuwa madarasa ya chini alijaziwaje na walimu waliopita.

Mwalimu wa Darasa la nne. “Ni mtoto mvivu, mchafu na hana marafiki. Hakusanyi kazi kwa wakati, japo akili anayo. Nampa alama D.”

Maoni hayo yalimfanya akunje uso, akiamini hakustahili hata hiyo alama D.
Ndipo alipoamua kuchukua karatasi ya kwanza, hii ikamduwaza sana.

Mwalimu wa Darasa la Kwanza. “ Iddi ndo mwanafunzi bora kwangu. Mwelewa, ana upendo, ametokea kupendwa na kila mwanafunzi hapa darasani. Ameongoza masomo yote kwa kupata alama A. Mimi nampa mtoto huyu alama A.”

Maoni hayo yakamfanya aiendee pupa karatasi ya pili.
Mwalimu wa Darasa la Pili. “ Iddi ni kijana mzuri, mpambanaji, hakubali kushindwa kirahisi. Katika watoto wasafi wa muda wote toka naanza kufundisha, kwangu Iddi namba moja. Kwa sifa hizi, nampa alama A.”
Maoni haya yakamshangaza zaidi.

Kama alikuwa namba moja kwa usafi pindi alipokuwa mdogo, kipi kimepeleka hadi kuwa mchafu na wakati akili zake zimeshatengamaa?

Alijiuliza wakati akiliendea karatasi la tatu.

Mwalimu wa Darasa la Tatu. “Sijashtushwa na matokeo mabaya ya Iddi kwa kipindi hiki, nafahamu mtoto anapofiwa na mzazi anakuwa katika hali gani. Iddi anahitaji uangalizi wa hali ya juu. Mimi nampa alama C.”
Karatasi hii ilimchoma moyo wake. Ndipo alipofahamu ni wapi Iddi alipobadilika na kuwa vile amuonavyo. Akaiwahi karatasi yake na kufuta alama F kwa wino maalumu. Akaenda sehemu ya Maoni na kuandika.
Niliwahi kuongopa kuwa nawapenda wote darasani, ila nimegundua kuwa moyo wangu umetokea kumpenda Iddi kuliko wote. Nampa alama A.
Baada ya kuandika hayo. Akaiweka karatasi hiyo kwenye file la Iddi.

Kilipofika kipindi cha Christ mass, wanafunzi walileta zawadi mbalimbali kwa mwalimu wao. Ni kawaida kwa Mwalimu husika naye kumpa zawadi mwanafunzi mmoja aliyeleta zawadi nzuri zaidi kushinda wote.

Katika zawadi zote zilizoletwa, Zawadi ya Iddi tu ndo ilionekana kufungwa rafu tena kwa kifungashio ambacho kilishatumika. Mwalimu alianza kuifungua hiyo kwanza.

Wanafunzi wenzake walicheka sana, hadi Iddi akakumbwa na fadhaa. Mwalimu akawanyamazisha huku akiendelea kufungua na kutoa vitu vilivyomo. Kwanza aliona bangili, mwalimu akaichukua na kuivaa hapo hapo. Hali iliyowafanya wanafunzi washangae. Hata Iddi hakutarajia hicho kitu. Zawadi ya pili na ya mwisho ilikuwa ni Perfume iliyobaki robo kwenye kichupa chake. Mwalimu akajipulizia na kuonesha kufurahi sana. Akazifungua zawadi zote kisha akawaambia wanafunzi wake. Wote mmeleta zawadi nzuri, ila Iddi ameleta zawadi nzuri kuliko wote.

Wanafunzi wote wakampigia Iddi makofi. Siku hiyo ndo ilikuwa siku ya kwanza kwa Mwalimu Elizabeth kuliona tabasamu la Iddi.

Wanafunzi wakabaki kimya kusubiri zawadi ya Mwalimu kwa mwanafunzi . Naye mwalimu akampatia Iddi Boksi kubwa lilifungwa vizuri. Iddi alipoenda kupokea zawadi. Alimwambia Mwalimu Elizabeth "Unanukia kama alivyokuwa ananukia mama yangu." Kauli hii ikamfanya mwalimu atabasamu.

“Utafungua nyumbani.” Mwalimu akamwambia na Iddi akaondoka na boksi lake huku wanafunzi wenzake wakiwa na hamu ya kujua zawadi zilizomo boksini.

Alipofika nyumbani, akafungua kwa pupa. Humo ndani akakutana na Sare mpya za shule, madaftari, kompasi na fedha tasilimu. Mwisho akakuta karatasi yenye ujumbe, akaichukua na kuifungua, akaisomoa moyoni.
Kwa kipindi chote nilikuwa sikujui, ila sasa nimejua kuwa wewe ni nyota. Sitaruhusu mwalimu mwengine akuhukumu kwa mwonekano wako. Kwa chochote utakachohitaji, njoo kwa mwalimu Elizabeth, atakusaidia.
Ujumbe huo ukamfurahisha zaidi. Akageuza nyuma ya karatasi na kuujibu. Kisha siku ya pili ambayo ndo ilikuwa siku ya maagano. Akampelekea mwalimu wake kikaratasi kile.

Mwalimu alitabasamu baada ya kuusoma ujumbe uliomo.
“Wewe ndo Mwalimu wangu bora wa muda wote.” ujumbe ulisomeka hivyo.
Shule zilipofunguliwa, Iddi akaanza Darasa la Sita akiwa msafi. Shule ikamtangaza kama mwanafunzi msafi kwa mwaka huo. Akamaliza la saba akiwa na rekodi ya kufanya vizuri darasani huku akiwa namba moja kwa Usafi. Akamtumia barua mwalimu Elizabeth. Akimwambia.

“Nimefundishwa na walimu wengi, bado wewe ni mwalimu wangu bora wa muda wote.”
Iddi alichaguliwa kusoma shule ya vipaji maalimu. Alipomaliza kidato cha nne, akamwandikia mwalimu wake Barua.

“Nashukuru nimepata ufadhili, hivi sasa nasoma kwa amani. Mbali na yote, sijawahi kukutana na mwalimu wa aina yako hadi hivi sasa. Hakika wewe ni Mwalimu wangu wa muda wote.”

Alipomaliza kidato cha sita, Baba yake Iddi akafariki. Kipindi hicho alishindwa kutuma barua kwa mwalimu wake. Alifaulu vizuri na kwenda chuo. Huko akafanikiwa kupata Degree. Akapata na mpenzi na wakafikia hatua ya kufunga ndoa. Alimjulisha mwalimu wake na kumwomba asimame kama mzazi wake kwenye harusi. Mwalimu alikubali. Na kweli, akabeba majukumu ya mama. Akawapa na zawadi maharusi.

Walipokua jirani, baada ya kutoonana muda mrefu, Iddi alishangaa kuiona bangili aliyompa mwalimu wake miaka mingi iliyopita, ikiwa bado mkononi. Na Harufu ya marashi, ni ile ile aliyomzawadia ingali ipo robo.
“Unanukia kama Marehemu mama yangu, hakika wewe ni Mama na Mwalimu wangu wa muda wote. Niliwahi kukuogopa, nikakuchukia. Leo nimeona faida ya kuwa na wewe karibu Mwalimu.” Maneno hayo yakamfanya Mwalimu amkumbatie kwa nguvu.

“Wakati naingia kwa mara ya kwanza darasani kwenu, sikuwahi kujua kufundisha kama ninavyojua sasa. Hakika umenifunisha jinsi ya kufundusha. Najivunia kuwa na Mwanafunzi na Mwalimu wangu wa muda wote.” Maneno hayo yakazua tabasamu na machozi ya furaha kwa wote wawili…

Naamini kuna cha kujifunza hapa.. Muwe na Siku njema ndugu zangu.
Kalamu Tulivu

HusseUMENIFUNDISHA KUFUNDISHA

Na, Christology
 
Upvote 2
Back
Top Bottom