Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
...hebu niwaulize nyie wana JF Tusaidiane mawazo, maoni na ushauri kuhusiana na hili.
Je?
Nini mtazamo wako mtu anapokwambia umemharibia maisha!
Tatizo nini? kwanini ujifikirie maisha hayana tena thamani bila fulani?
Tujadili kwanini kinyongo, chuki, fitna, wivu, hasira, yakichanganyika na mapenzi yanachangia walio wengi kupoteza matumaini ya maisha.
Je, utauchukuliaje msiba wa aliyekuwa wako, aliyejiua sababu "umemharibia maisha!," au,
Je, unamchukuliaje mwenza wako ambaye anakwambia atajiua kwani maisha yake hayana thamani bila wewe?
Nini suluhisho kukabiliana na 'mtihani huo'
Kwa wenye mioyo dhaifu, natanguliza ombi la msamaha kama nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja au nyingine.
Nataka kuamini kwamba kila mmoja wetu amejaaliwa utambuzi na uchaguzi.
Unapochagua, ina maana pia unajikubalisha matokeo yatayotokana na maamuzi yako.
Kumtupia mwenzako lawama ya "amekuharibia" ina maana hukuwa makini kwenye utambuzi na uchaguzi wa
maamuzi yako.
Ni jinsi gani twaweza boresha utambuzi, uchaguzi na maamuzi yetu kwenye maisha na mapenzi kwa ujumla?
WHAT DO YOU WANT IN LIFE?