Umeniharibia maisha! ...what?


MTM Spot on track bro!

maisha ni "kitendawili, kitegue....!"

,...pamoja na kuwalaumu kwetu hawa wanaotwambia tumewaharibia maisha?
hao ni wenzetu, wake zetu, ndugu zetu, wafanyakazi wenzetu etc....je, tuwasaidiaje?
nadhani kuwatenga kutawafanya wafiche makucha yao kwa muda...

...tayari wana disability ya kujiona wao wanakuwa victimized bila ku own their faults kwenye relationship.
Hudhani kwamba ku boost ego, pride na self esteem zao ni njia mojawapo ya kuwasaidia? hebu tupe darasa
la mental heath sasa.... kama jamii, tunakosea wapi kwenye malezi?

iwapo mke (mama) ndiye mklezi wa taifa la kesho, huoni kwamba tukiendekeza 'ulemavu' huu tunazidi kuzalisha
whingers, whinpers and moaners nchini?
mfano; cheki thread za kumlaumu Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, LOL...
hawaishii hapo,....mpaka majumbani wao ni kulalamika tu!

Where do we draw the line and take up the responsibilities za maisha/mapenzi?
 
bro, some of the best approaches in healing couples challenges is role switching, couples retreat (karibu tunaandaa moja in august), and open talks where we agree on everyones roles in a problem

in many cases they refuse to bulge, but a fter a week you will find that you sit together and admission comes so easy, especially after 'quality time' - :bange:
 
Reactions: Mbu
Mkuu watu hatuishi kwenye (Vacuum) tunategemeana ili kuweza kuendesha maisha ya kila siku. Sasa iwapo mtu alikuwa kwenye straight line kabla ya kukutana na wewe na for your influence unamsababisha kwenda astray.., then ni kweli umemwaribia maisha..., mfano mzuri ni kwa wale wanaowapa wenzao mimba na kuwatelekeza.., au kuwa-abuse emotional na kuwafanya wawe tofauti na mwanzo..,

Mkiwa wawili inabidi kutegemeana sasa badala ya kumyanyua mwenzako akianguka wewe unamsukuma then utakuwa responsible for his/her failures..., mfano mzuri ni Whitney na Bobby; lazima tutapoint a finger kwa Bobby Brown kumfanya Whitney aanze kubwia unga cause kabla hawajakutana Whitney hakuwa hivyo..., au wale wanaowapa karaha wenzao na kuwasababisha waanze ulevi..

Yes ni kweli Binadamu wote tunao uwezo wa ku-influence maisha ya watu tunaowazunguka na action zetu za bila busara zinaweza kupelekea kuharibu maisha ya wenzetu
 

Mi nawaonelea huruma sana wadada kwa hii kadhia . . . sijui inachangiwa na KUPENDA MTU ASIYEMPENDA??!!!
Ila kwa asilimia fulani naona matatizo huanzia kwa binti mwenyewe.
Kikawaida sisi wanaume hatuna mapenzi ya PAPO KWA PAPO, huwa tunaanza kutamani kwanza.

Achilia mbali hao nilioelezea awali kwamba walitaka kujiua kwa ajiri yangu (hawa sikuwahi kushiriki nao mapenzi), kuna binti mmoja nilieanza nae uhusiano tangu 2007. Alikuwa 18yrs mwaka huo na kusema kweli mwanzoni nilianza kwa kumtamani tu, sikufikiria future yoyote na yeye.
Na mi nilikuwa mwanaume wake wa kwanza kushiriki nae mapenzi.

But as times goes, taratibu nikaanza kuvutiwa nae, ukarimu wake, upole wake, uelewa wake, kujishusha kwake (hata kama mimi nina makosa yeye hujishusha always) na hatimaye mapenzi ya dhati aliyonayo kwangu.
Kuna wakati tunapanga tukutane, lakin ghafla inafika siku yenyewe mama ake anaumwa, anahitaji mtu wa kumpikia, basi akiniambia nakuwa mbishi kuelewa, naanza kumshutumu kwamba hanipendi, kapata mtu mwingine. Basi binti wa watu anajitolea, ananibembeleza naelewa hatimaye namuelewa.
Kuanzia hapa nikajiapiza "Huyu ndie waifu mwenyewe" lakin sikuwahi kumwambia.
Nikaanza kumsikiliza kila anachoniambia, akiishiwa na pesa ya matumizi namtumia kwa bank (M-pesa bado kuanzishwa wakati huo)
Then nikaanza kumtumia kwa M-pesa kuanzia 50,000/=, 100,000/= n.k.
Niliji-commit kwake moja kwa moja tangu wakati huo.
Then Mwaka huu mwanzoni mambo yakabadilika . . . .
 

VoiceofReason many thanks kwa kutuletea maoni tofauti,
hiyo ya Whitney na Bobby imenichekesha sana. Dah, mdahalo unanoga,....

...kama alivyoandika MTM, njia mbadala ni kuwa encourage partners ku switch roles,
nimeipenda sana. Wapi mnafanyia hizo workshops? nahisi hiyo inasaidia ku encourage 'empathy!'(?) ndio wajibu/huruma?..

nadhani mfumo dume, unaotokana na mila, desturi na tamaduni zetu unachangia kwa kiwango kikubwa pia
mwanaume kujijengea ukuta (kuto bend the rules) asijeonekana 'amekaliwa' aka 'Mume *****' aka 'amewekwa kiganjani!'

Matokeo yake ndiyo hayo kama VOR alivyoyaongelea, mtu anageuka psychological abuser na mwenzake ili kum- accomodate anajivisha joho la u victim mpaka siku anapodata, ndipo utasikia 'Umeniharibia maisha!'...

Kwa upande wa pili, mwanamke anapokutana na mume ambaye anampa uhuru wa kujiamulia maisha, uhuru wa maamuzi nk...(iwapo background yake haikum shape kukabiliana na mume wa aina hiyo,) utakuta through her confusion anavuka mipaka ya ndoa... akishanogewa na huo uhuru na utapojaribu mrudisha mstarini, kasheshe lake kama ni mashua basi huenda chombo kikazama.

Sasa hapo ndipo nami ninapokwazika, Uhuru uliotumiwa vibaya ni kosa la nani?
Mke amejiharibia maisha, au mume kamuharibia mke maisha?
 
Mbu topic nzuri sana, huwa nafikiria niwe nawasiliana na wewe kwa ushauri maana unajua sana ku-analyse haya mambo!

Naamini yote niliyopitia ni changamoto za mapenzi...nimejifunza pia kubeba lawama zangu pia kujipa moyo kuwa sikuzaliwa na huyo mtu nimekutana nae tu katika safari hii ya maisha hivyo lolote linaweza kutokea..

Watu wengi huhisi kuharibiwa maisha kama walipotezewa muda na wapenzi wao tena makusudi bila kujali hisia wala upendo juu yao...mara nyingi wanagutukia too late kuwa walipotezewa muda!!
 
....Niliji-commit kwake moja kwa moja tangu wakati huo.
Then Mwaka huu mwanzoni mambo yakabadilika . . . .

ha ha haaahhaa!....mbona unakatisha uhondo? mwenzako nilikuwa nishavuta kiti hapa,
hebu endelea yaliyokusibu!, enhe!...
 

vice.. i may agree with you ila nina wasiwasi kwamba mfano wa mimba siyo wenyewe... kumbuka hukumbaka, na mwanamke anajua cycle ya mayai yake

ungejua maana ya kumuendeleza mwanamke ni kuendeleza jamii, ungekubaliana na mimi kwamba mwanamke ndiyo anayerun maisha yetu; to me mimba, mtu kubadilika na kuwa malaya, mlevi au mimba ni vitu ambavyo subconsicously anakua anaona yanayotokea na kupiga moyo konde

BTW, nikimpa mimba mwanamke bila kupanga, si kwamba nimemharibia maisha, bali tumeharibiana maisha kwani kuna majukumu ya kulea yanaongezeka na kwa sisi tuliooa ni kwamba tunaongeza challenge ya pili nyumbani ya kuleta mwana wa nje (si mwanaharamu)

we have to balance the cards to be fair, as long as hakubakwa au kulazimishwa, basi anashare 50% of responsibilities... and that is also a way of empowering women
 

Anytime BJ, you know where and how to contact me.
Anytime!
 
Mbu!..
Maisha yana mabonde na miinuko... Kamwe maisha sio tambalare... Hakuna mtu anayeharibu maisha ya mtu... bali inabidi watu tujifunze kukubaliana na ukweli wa hali halisi kwamba matatizo hayo ndiyo maisha yenyewe 'kupata mimba na kukataliwa ndiyo maisha yako.' Maisha hayaharibiki labda tuseme yanaenda ambavyo mtu hatarajii yaende!..
 
Reactions: Mbu

mmnnhhh,

Kamanda MTM, nadhani kina dada wengi hata wa humu JF watakuja wakali hapo kwenye wadada wanajua cycle ya mayai yao. Ni mara ngapi ushasikia tarehe zimebadilika? Nadhani kwenye suala la mwanamke kupata mimba nasi wanaume tunapaswa tuchukue jukumu la lawama. Nawasifu sana wale kina dada ambao at all cost kuepusha hili watalazimisha matumizi Condom.

Mwanaume, iwe ni boyfriend au mume nadhani nasi tunapaswa kujifunza menstruation circle za wenzetu, ...nasi tukajua zipi ni Ovulation days, zipi ni danger days na zipi ni safe days...kumwachia mama/au "mchuchu" jukumu hilo ni sawasawa na kuchezea shilingi chooni. Je, akikutega...?

Suala la mtoto through unplanned pregnancy inaniwia ngumu na uchungu kuita hiyo ni "kumharibia mtu maisha."
Am always anti Abortion. Nipo makini sana linapokuja suala la kufanya mapenzi bila kinga. Inapotokea mwenzangu amepata ujauzito, nauchukulia ujauzito huo +vely, ...ni blessing ya mapenzi yetu. It happenned to me, na nilimu- encourage partner wangu azae, na hivi leo na mtoto mkubwa ninayejivunia.

Unless kuna mtu atakuja na definition nzuri, i.e mwenyewe alijipangia nini mpaka unplanned occurance ndio iwe sababu ya kumlaumu mwingine amemharibia maisha! Kabla ya hapo, ajiulize wakati wa kufanya uchaguzi wa maamuzi yake, alifikiria faida na hasara ya tendo lake, au aliingia kichwa kichwa tu?
 

ha ha haaahhaa!....mbona unakatisha uhondo? mwenzako nilikuwa nishavuta kiti hapa,
hebu endelea yaliyokusibu!, enhe!...

Kwanza akaanza na uchokozi eti " Siku hizi hunipendi, niliwahi kukupigia simu nikasikia sauti ya mwanamke anapokea . . . . "
Nikamwambia hakuna kitu kama hicho, Na anajua wazi simu yangu hata niwe na Maza hawezi kuipokea, sembuse mwanamke mwingine.

Then akaanza: "CPU unanipenda kweli? Nyie wanaume mnataka kutuchezea tu basi, lengo lenu ni kupata kidude tu, then uniweke mimba ukimbie"
Nikacheka kwanza, then nikamjibu: "Naomba utafute siku nije kwenu nijitambulishe, na baada ya hapo ntakuleta kwetu"
Akafikiri mzaha, nikakomaa nae kwamba akishamaliza mitihani yake na kufunga chuo, nataka mguu wake mguu wangu moja kwa moja mpaka kwao.

Alivyoona nimekuwa serious, akaanzisha ligi nyingine: "Unajua CPU mi nasoma saa hizi, hata kama ingekuwa ndo wewe mdogo wako anasoma then amlete mwanaume kujitambulisha, si ataonekana hataki shule??? Basi subili nimalize kwanza"
Nikamwambia sawa, ila asilalamike kwamba sina future nae tena.

Then akaja na kisingizio cha mwisho ambacho ndo kilinimaliza. Unajua alisemaje??!!
"CPU unajua sisi kwetu ni masikini sana, ndugu zangu wengi hawana kazi, kwahiyo kama unataka kunioa itabidi ukubali KUGHARAMIA NDUGU ZANGU WOTE"!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nilimuuliza maswali yasiyokuwa na idadi kutokana na hii hoja yake lakin akaishia kusema tu, "Kama utakubali kugharamia tu, vinginevyo itakuwa ngumu" Basi nikamwambia ruksa kumtafuta masikini mwenzake au tajiri atakae kubali kugharamia ndugu zake.

Then rudi kwenye hoja ya Tulizo uoanishe na haya maelezo yangu.
 

ni kweli swahiba

ilaa issue yangu hapa was precautionary... kwani hata kama cycle inayumba vipi huwa tunashauri kitaalam watu wapige wider range ya siku na hata kinga au kumalizia nje, my main point there was a woman akiamua usimfanye au kumwaga ndani, basi hutafanya hata ujitahidi vipi??

unless ni rape --- definition ya rape is soo wide these days

sasa tukija hoja nyinge, i agree with you completely
 
MTM na Mbu..., ninakubaliana na nyie 100% kwamba ni vizuri badala ya kupoint fingers tuwe tunajiangalia wenyewe..,

llakini point yangu ni kwamba "Behind every successful man there is a woman and vice versa is true..., ni kwamba in order to reach our potential lazima tupate support ya mtu and there is nothing better kama support ya mtu mnayeshare emotions.., ni kwamba huyu ni kama umempa your heart and he/she can make you or destroy you...., mfano mwingine Lauryn Hill (since ameolewa na yule bwana) she stopped pursuing her music career and the man has turned her into a house wife although she was a career woman... (ingawa angeweza kumsupport na angeweza kufanya vyote)

Ingawa kuharibu maisha its too bigger a word.., lakini am sure most of us kama tukiwapa support wenzetu kwa mambo wanayoweza kufanya effect yake inaweza ikawa better.., mfano wa mimba kama mtu atakubali kuwa mtoto ni wake na ku-offer support then its okay lakini pale anapomkataa mwanamke na kusema mtoto sio wake hapa atakuwa amempa mwanamke mzigo...
 

Pheeeeeeewwwww!.....well, well, well....kwa hapo kweli nimeona wapi "tofali" aka "Jiwe la msingi" la umeniharibia maisha lilitaka kuwekwa rasmi!

Nimekosa hata cha kuongeza bana, pole sana kamanda.

 

....okay, nadhani in a nutshell unaongelea utegemezi!....Support in terms of moral, emotional, financially, etc au sio?
Umesisitiza hapo kwenye emotional, kwani ndipo tunapogusa ego, pride, self esteem nk....mtu anavyoweza jiskia yeye ndio yeye...uki break down hapo una justify "kuharibikiwa maisha?"

Kwa uchambuzi huu, naamini tunarudia kule kule kwenye tahadhari za ku bank emotions zote kwa mwenza wako.
Hii inasaidia kuokoa ile 'emotional blackmailing.' Au wenzangu mna mtazamo gani?
 
Endelea bwana CPU umekatisha uhondo
 
Hii nyuzi imekwenda shule mkuu, asanteni sana kwa michango yenu iliyojaa busara, hata wengine kutoa uzoefu wa maisha yao binafsi. Sijaona kama JF.

Kwa maoni yangu kuharibiana maisha kupo tena sana. Ila kusema ati nitajiua ukiniacha hilo tena ni tatizo lingine linalohitaji tiba. Huku kijijini kwetu saa hizi ni usiku na dowans hawajatufikia bado, kesho nitatembelea mjini kuendeleza libeneke.

Mlale unono bila kusahau chandarua maana MBU ni wengi kweli.
 
Reactions: Mbu
When you lead someone on a path knowing very well the end won‘t be pleasant for them ,you sure like hell deserve credit for it.Watu wengi wanawake kwa wanaume wanapoingia kwenye mahusiano kwa sababu ambazo ni za kibinafsi mf. sex...pesa...sifa na mengineyo hua wanajua vizuri sana kwamba baada ya wao kupata walichotaka na kuridhika lazima watakua wamewakorofisha/wachanganya wale waliotumiwa kutimiza haja na mahitaji yao kwa namna moja ama nyingine.

Mwanaume/mwanamke anaeingia kwenye mahusiano kwa sababu hizi za kibinafsi alafu akamwaminisha mwenzake kwamba anampenda na ana malengo nae mwenzake anajitolea mengi kuhakikisha mahusiano yao yanachanua.Muda...pesa...marafiki au hata ukaribu wa ndugu unaweza kutolewa kafara kwaajili ya hili alafu siku ya siku mtu anakwambia “bwana ehhhh mi nimeshakuchoka“ au “sikupendi tena“ na kama kaamua kukumaliza anakwambia kabisa “nia yangu ilikua kupoteza muda tuna wewe huku nikisubiria wa kunifaa...pole/samahani kwa kukutumia“.Muda ulishaenda...waliokupenda kweli ulishawatolea nje sasa nao hawakuhitaji tena...marafiki ulishapoteza kadhaa kwasababu ya mpenzi....pesa ulishatumia nyingi kumsomesha/kumfungulia biashara then unajulisha/gundua kwamba wote ulikua mchezo tu....KWANINI USIONE KWAMBA UMEHARIBIWA MAISHA???!


Mwanaume au hata mwanamke aliye ndoani anapomwaminisha mwenzake yeye ndo yeye kumbe mkewe/mume yuko shule au kamuacha nyumbani mpaka mwenzie anakolea na kuamini ndoa itakuwepo ni muda tu na mipango...ghafla mimba imenasa alafu anakuja ambiwa “nna mke/mume mimi ujie“....na miaka ilishakata hisia zilishachezewa KWANINI HUYU MTU ASIONE KWAMBA KAHARIBIWA MAISHA in terms of malengo na mipango???!

Mume/mke au mchumba yuko mbali anatuma vijisenti kila mwezi angalau nao siku moja wawe na kwao alafu anarudi kukuta pesa zake zilikua zinamlisha mwanamke/mwanaume mingine au imejengwa akifika anaambiwa hana chake anaingizwa mwingine ndani KWANINI HUYU MTU ASIONE KAHARIBIWA ukizingatia kwamba hata viakiba vyake alivitoa akijua faida ipo?!

Yapo mengi sana yanayompa mtu ruhusa/haki ya kuona ameonewa au hata kuharibiwa malengo na mipango yake aliyojiwekea awali.Ndio kwa kiasi flani hata mkosewa anaweza kua amechangia kwa kutokua wangalifu ila ni wangapi kati yetu wenye bahati ya kufikiria kwa kutumia kichwa badala ya moyo linapokuja swala la kuanguka mapenzini?!Sio wengi....na ndio maana mioyo haiishi kuvunjwa kwahiyo usihukumu kila anaesema hivyo kwamba ni uzembe wake....jua kwanza historia ya aliyomkuta.

Kuhusu wanaoitisha kujiua kwakweli nashukuru sijakutana nao....ila hua najiuliza hua wanapoamua kujia kweli hua wanapania kumkomoa nani haswa maana namjua mzee aliyejiua kwaajili ya mapenzi na mpaka leo hua hata siwezi kuimagine yule mama na wanae watakua wanajiskia vipi kujua yeye ndo msababishi a watoto kujua mama ndie msababishi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…