Umeniharibia maisha! ...what?

Yaani kweli kabisa mwanaume anapaswa kujua mzunguko wa mwanamke wake, kuna wakati sie nasi ni ving'ang'anizi sana mwanaume akiwa strong anakataa kabisa kukutana siku hizo mbaya, nakumbuka mie nilikuwa siwezi kabisa kuhesabu siku zangu hatarishi ila bf wangu ambaye sasa ni mume alikuwa kipaumbele kunihesabia ili nisipae ujauzito, ila kuna siku nang'ang'ania utadhani nini sijui inabidi jamaa ajitahidi mwishowe aruke vihunzi lol mtoto nilikuwa mbishi hatar, sasa hapo ningepata ujauzito ningesema nimeharibiwa maisha kweli
 

HA HA HA!

...we mwana wee....ulikuwa unang'ang'ania eeh?!

Anyway, kusema ungekuwa "umeharibiwa" wakati mwenyewe ulikuwa unang'ang'ania hiyo ingekuwa unakataa responsibility ung'ang'anizi wako!

Ulikuwa unataka kujiharibia maisha bana, thx God shemeji aliliona hilo na mapema.
 
Kuna wanaume wako makini sana aisee
 
Duh inaonekana ulikuwa mtundu enzi zako
 
.
Kwa uchambuzi huu, naamini tunarudia kule kule kwenye tahadhari za ku bank emotions zote kwa mwenza wako.
Hii inasaidia kuokoa ile 'emotional blackmailing.' Au wenzangu mna mtazamo gani?
Yeah thats the way....., lakini if only it was that easy....., Easier Said than Done...... and the facts remains.....
"Those we Love the Most, Hurt us The Most......"
 

Lizzy! am impressed na analysis yako...!
Kwakweli umeitafsiri 'kuharibiwa maisha' vizuri mpaka nimeshawishika kukubaliana nawe.
Ngoja nitafute loopholes kwenye maelezo yako, usisahau na kajiasili ka ubishi!

 
Ukiipata hiyo loophole kwa hili bandiko nitaamini kweli u mmanyema kwa ubishi
 
Reactions: Mbu
Khaaa!!! huu uzi mpaka uwe umeenda shule... teh teh teh
 
Hakuna wa kuharibu maisha ya mwenzie, kutokujua kusoma alama za nyakati ndiyo kunakufanya une umepotezewa muda. Hivi kweli kwa karne hii mwanaume au mwanamke anaweza kukupotezea muda? kivipi?

Wanawake bwana tuna matatizo mengi tu, sometimes mwanaume anajitahidii kukuonyesha kwamba hakutaki wewe unajida huoni end of the day unasema umeharibiwa muda wako? Acha ujinga na upumbavu, soma alama za nyakati, ukiona vipi kula kona mapemaaaa, na wanaume vivyo hivyo usipoteze muda kwa mtu asiiyekupenda.

Siyo lazima nikwambie sikutaki, vitendotu vikufanye uwe na uelewa wa ziada. Pole sana wale mnaopoteza mida halafu mnasingizia wenzenu eti wamewapotezea muda.
 
Lizzy! am impressed na analysis yako...!Kwakweli umeitafsiri 'kuharibiwa maisha' vizuri mpaka nimeshawishika kukubaliana nawe.Ngoja nitafute loopholes kwenye maelezo yako, usisahau na kajiasili ka ubishi!
Hahha...Mbu embu weka Umanyema bench leo tu maana ukizipata ntaharakisha kuziziba yani utakesha hapa leo!!!
 
Ukiipata hiyo loophole kwa hili bandiko nitaamini kweli u mmanyema kwa ubishi

LOL! ...huyu Lizzy mjanja sana, amefunika loopholes zote kwa sentensi hii ;

ni wangapi kati yetu wenye bahati ya kufikiria kwa kutumia kichwa badala ya moyo linapokuja swala la kuanguka mapenzini?!Sio wengi....
...in other words, ameturudisha kwenye lawama ile ile ya uchaguzi wa kutumia akili badala ya kuusikiliza moyo wengine husema 'roho,' ---moyo ambao hutoa tahadhari kutokana na past experiences....

Jamani, sote tumezaliwa na sixth sense,...kuna mambo na ishara utaoteshwa ndotoni,...kuna mambo roho itasita,...iwapo uta overrule ishara zote hizi, halafu lawama ukaenda mtupia Lizzy kwa 'kukuhakikishia' mapenzi kumbe ni usanii, itakuwa unakosa kuchukua responsibility ya maamuzi yako!...

hebu chukulia mfano huu;
  • Kipofu haoni, lakini anaiamini fimbo/mbwa wake!
    ...
  • Chumbani kwako; funga mapazia, zima taa, kisha jifunge kitambaa machoni kisha utafute mlango utoke...
Tuna macho, pua, mdomo, masikio na viungo kamili lakini tunajisahau jinsi gani vyote hivyo vinavyotambua hisia, itakuwa
hisia ya amani, hatari, tahadhari nk ambavyo ni roho tu yenye uwezo wa kutambua?...Huu ni utambuzi kwenye Spiritual level...!

Listen to your instincts, ingawa si kila tahadhari inaashiria hatari....!
Baada ya 'kutendwa' utamsikia mtu anakumbukia, "tena nilihisi mimi basi tu nikapuuzia...!"
 
Hahha...Mbu embu weka Umanyema bench leo tu maana ukizipata ntaharakisha kuziziba yani utakesha hapa leo!!!

if there comes a day nikamlaumu wife wangu kwamba kaniharibia maisha, basi ntakua nina matatizo makubwa coz i participated in the process

and if she come and say nimemuharibia maisha.... ntakubali coz women are alwayd right!!
 




umeongea poa MJ1,
Hebu angalia na hii signature yako,
kisha itafakari katika huu mustadha wa ''Umeniharibia maisha''

.............Give more love, than what you receive........................
Mjukuu Mtiifu; 2011


 


..............ubarikiwe kiongozi, umegota kwenye ukweli kabisa.............
good analysis..............
 

Mbu umenigusa hapo kwenye kijani- nafikiri kwa kuwa zamani kulikuwa hakuna mwingiliano mkubwa kama sasa, wazee wetu walikuwa na kitu tunaita Social intercorse...yaani unakuwa hujaonana na mtarajiwa wako lakini alikuwa tayari anafahamika kiukoo (hao wake/waume watarajiwa walikuwa wanachaguliwa kutoka katika koo zilizokuwa zinafahamika) so hata ukimwuoa unakuwa (na jamii nzima) inaelewa kuwa ana tabia nzuri na hatokusumbua. Sasa hivi tunakutana katika michanganyiko ya kila aina, mwingiliano wa makabila, matabaka kila kitu umekuwa mkubwa sana si rahisi koo kwa koo zikafahamiana kiviiiile, so ni muhimu kuchukua muda kufahamiana na mwenzio
2. Maadili pamoja na 'upofu' wa uhuru na haki za kijinsia uliwafanya mama zetu kuwa na uvumilivu wa hali ya juu. Nimeweka upofu kwenye quotes kwa sababu ni upofu ambao ninaamini kuwa ulikuwa na faida sana katika kudumisha ndoa na maadili ya kipindi kile. Kizazi cha sasa sie kwanza maadili hakuna- tunalelewa na 'ulimwengu' na si jamii au familia kama walivyobahatika wazee wetu. Pili 'akili' ya kuwa mimi ni huru, nina haki sawa na mwenzangu, asinibabaishe .....ndio inayopelekea tuwe makini katika kupata mwenza.

Kuhusu muda gani tutumie, hiyo ni subjective to wahusika kwa sababu mnawezachukua hata miaka, kama kuna mwenye hila anawezaificha hadi mkioana (ingawa mie huwa nasema ukiamua kumchunguza mtu utamjua tu) sema kipindi hicho ambacho wengi wetu tunafikiria ni cha kuchunguana hujisahau na kukifanya ndo kipindi cha kujaribu maisha ya ndoa!! Utakuta wakati wa uchumba mtu anafanya madudu lakini badala ya mwenza kukaa na kuyatafakari yale madudu na kuchukua hatua..yeye analia na kusamehe kwa kujifariji kuwa ....tukiingia ndani atabadilika!
 
Reactions: Mbu
umeongea poa MJ1,
Hebu angalia na hii signature yako,
kisha itafakari katika huu mustadha wa ''Umeniharibia maisha''

.............Give more love, than what you receive........................
Mjukuu Mtiifu; 2011



bacha kweli kabisa hiyo give more love than what you receive kwa upande mmoja ndo screw diver iwapo unapogive unategemea return sawa! kama ukigive na kutegemea akupende zaidi (asikutende) basi ikiwa kinyume chake ni wazi 'umeniharibia maisha' inaweza ikatokea BUT if you give more than what you expect from him/her hata akikutenda utashukuru kwa kusema I did what I could, haikuwa riziki yangu na pia utaishia kujilaumu tu na si kumlaumu!!
 
Jaman jana tu mwenzenu aliyekuwa mpz wangu wa miaka kansalit na mwaka huu ndio nimefanikiwa fanya nae mapenzi kwani alikuwa bikla na tumefanya tendo hili mara 2 tu chakushangaza mwezi ulio pita alisafili kwenda hom kwao kwan tuna kaa wilaya tofauti baada yakufika huko nikapigiwa sim na aliwekuwa mpz wake wa zaman kabla yangu akiniambia kuwa mpnz wangu ana tembea na rafiki yake na siku ana piga cm aliwakuta mara ya 3 wakitoka guest house mi nikaamua kumuuliza akanijibu ni maneno tu ya watu alafu hapo hapo akampigia sim jama aliyenipa taarifa na kumtukana sana kisha aka mpigia huyo jamaa yake mpya kumuuliza kama ameniambia japo mimi hatufahamiani sasa mtu kama huyu haja nialibia kweli tumekuwa wote kwa miaka 3
 

............Dwork1 sasa hapo umeharibiwa maisha gani?
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…