Umening'iniza rozari au tasbihi kwenye gari lako lakini hupishi wenzio, huo ni urembo?

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Unakuta kwenye gari imening'inia rozari au tasbihi kuonesha mwenye gari - labda kama ni mwajiriwa - ana mtukuza Mungu ambaye anamtaka ampende jirani yake.

Jirani ni mtu yeyote aliye karibu yako. Sasa inakuwaje umkatarie mtumiaji mwingine wa barabara kuingia barabara kuu au kutoka barabara kuu? Pia, iweje uwakatallie watembea kwa miguu kuvuka barabara?

Sasa hiyo rozari au tasbihi ni urembo? Maanake kama ingekuwa inakukumbusha kuwa mtu mwema basi tungeuona wema wako kwa vitendo.

Kwa mlioweka misalaba, rozari, tasbihi, picha za mambo ya dini, naomba mniambie mmeweka ishara hizo za ucha Mungu wakati matendo hamna ni kwa ajili ya nini?
 
Unakuta kwenye gari imening'inia rozari au tasbihi kuonesha mwenye gari - labda kama ni mwajiriwa - ana mtukuza Mungu ambaye anamtaka ampende jirani yake...
Wanaamini ni kinga!
 
Unakuta kwenye gari imening'inia rozari au tasbihi kuonesha mwenye gari - labda kama ni mwajiriwa - ana mtukuza Mungu ambaye anamtaka ampende jirani yake...
Moyoni mnafiki, machoni rafiki ni mbwembwe tuu mkuu!
 
Ni dhalau tu kama dhalau nyingine bongo kila mtu mjuaji. Imagine mtu una degree mbili unakolomewa getini na mlinzi darasa la pili B. Au mwenyeki wa mtaa ambae hakunaliza hata elimu ya watu wazima, Hapo sasa umejishusha hutaki ajuwe kama umesoma au ni kiasi gani unajuana na boss wake.

Bongo bana.
 
Sioni shida hapo kama mtu una haraka zako au sehemu kumpisha mwezio sio rafiki
 
Unakuta kwenye gari imening'inia rozari au tasbihi kuonesha mwenye gari - labda kama ni mwajiriwa - ana mtukuza Mungu ambaye anamtaka ampende jirani yake. Jirani ni mtu yeyote alliye karibu yako. Sasa inakuwaje umkatarie mtumiaji mwingine wa barabara kuingia barabara kuu au kutoka barabara kuu? Pia, iweje uwakatallie watembea kwa miguu kuvuka barabara?

Sasa hiyo rozari au tasbihi ni urembo? Maanake kama ingekuwa inakukumbusha kuwa mtu mwema basi tungeuona wema wako kwa vitendo.

Kwa mlioweka misalaba, rozari, tasbihi, picha za mambo ya dini, naomba mniambie mmeweka ishara hizo za ucha Mungu wakati matendo hamna ni kwa ajili ya nini?
Tumefikiwa ..... Mi na ning'iniza kwenye bajaji.....
 
Unakuta kwenye gari imening'inia rozari au tasbihi kuonesha mwenye gari - labda kama ni mwajiriwa - ana mtukuza Mungu ambaye anamtaka ampende jirani yake.

Jirani ni mtu yeyote aliye karibu yako. Sasa inakuwaje umkatarie mtumiaji mwingine wa barabara kuingia barabara kuu au kutoka barabara kuu? Pia, iweje uwakatallie watembea kwa miguu kuvuka barabara?

Sasa hiyo rozari au tasbihi ni urembo? Maanake kama ingekuwa inakukumbusha kuwa mtu mwema basi tungeuona wema wako kwa vitendo.

Kwa mlioweka misalaba, rozari, tasbihi, picha za mambo ya dini, naomba mniambie mmeweka ishara hizo za ucha Mungu wakati matendo hamna ni kwa ajili ya nini?
Jirani ni mtu yeyote aliye karibu yako ❌ bali Jirani ni mtu yeyote anayehitaji msaada wako✔️
Mkuu; Usidanganyike na uwekaji wa misalaba, rozari n.k. n.k. Huo ni Ufarisayo. Hao ni Mafarisayo (Japokuwa sio wote). We angalia tu matendo yake kama kweli yanashabihiana na kile anachotaka kionekane machoni pa watu.
 
Back
Top Bottom