Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 577
UMEONA RAIS SAMIA ANAPIKA KWA NISHATI SAFI⁉️
Leo nimeona kipindi TBC Rais Dkt Samia akipika kwa kutumia nishati safi ya umeme na gesi. Kitu ambacho ni nadra na nadhani hakijawahi kutokea kwa Rais yeyote nchini kama sio Afrika nzima.
Shirika letu la TAA tunaoratibu kampeni ya kupanda miti ya SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA tumekoshwa mno na kitendo hiki cha mfano wa kuigwa.
SOTE tuachane na mazoea ya kutumia nishati chafu za kuni na mkaa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.
Aidha tukiachana na mabadiliko ya tabianchi, mkaa na kuni kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO huua karibu watu milioni 4 kote ulimwenguni kabla ya wakati, huku nchini inakadiriwa watu 33,000 hufa kila mwaka kutokana na matumizi ya nishati chafu ikiwemo mkaa, kuni, mabaki ya mazao kama vile magunzi ya mahindi na kinyesi cha wanyama.
Takwimu hizi zinaonyesha hali ni mbaya kuliko watu wanaokufa kwa, Malaria na hata kifua kikuu.
Mkaa kimsingi ni kaboni tupu, na mkaa unaochomwa hutoa viwango vya juu vya kaboni dioksidi, kaboni monoksidi, na vichafuzi kama vile masizi, ambavyo vinaweza kuingia ndani kabisa ya mapafu, hasa katika majiko yasiyokua na sehemu za kutolea hewa ya kutosha na kusababisha vifo ama kuharibu macho na kuwa mekundu na kupelekea kuuawa vikongwe kwa kuhofiwa wachawi katika baadhi ya makabila nchini na Afrika kwa ujumla.
Kwa sasa ni asilimia 6.7 tu ya kaya ndio wanatumia nishati safi, hivyo tukianza kutumia nishati safi tutaokoa maisha yetu na kuokoa takribani dola bilioni 1.4 duniani za kila mwaka zinazotumika kuwatibu wanawake walioathirika kiafya kutokana na matumizi ya kuni na mkaa, tutaokoa dola milioni 800 zinapotea duniani kila mwaka kutokana na wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni badala ya kufanya shughuli za kuingiza kipato.
Nafahamu wengi tungependa kutumia nishati safi mbadala kama alivyotuonesha Rais wetu ila tunahofia gharama.
Rais wetu ametutoa hofu.
Kupitia kipindi cha Pika kijanja kilichorushwa TBC leo Septemba 08, 2024 Rais wetu ametangaza hatua mbalimbali ambazo Serikali imeanza kuchukua kupunguza bei ya nishati safi; ameagiza kupunguzwa kodi katika nishati safi, taasisi zote za umma zenye zenye kulisha watu zaidi ya 100 kuacha kutumia kuni na mkaa tangu Januari 2024 badala yake kutumia nishati safi, pia elimu itolewe kuelimisha wananchi kwamba nishati safi sio gharama kama nishati chafu mfano umeme wa Tsh 200 unavisha makande tena kwa muda mfupi kuliko mkaa ambao ungehitajika wa Tsh 1000.
Enyi watanzania wenzangu,
Shirika la TAA linawaomba kwa unyenyekevu mkubwa kuachana na matumizi ya nishati chafu na kuanza utamaduni wa kutumia nishati safi na kupanda miti kwa wingi na kumuunga mkono Rais wetu Dkt Samia kukomboa afya na uhai wetu na kuifanya dunia yetu kuwa sehemu nzuri na salama ya kuishi dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Suphian Juma Nkuwi,
Mkurugenzi Mtendaji-TAA
Simu: +255717027973
Email: singidakijani@gmail.com
View: https://x.com/SuphianJuma/status/1832765991828209670?t=Izp23STlUrPzmKhPKl5SVw&s=19