Umeshawahi au kunusurika kwenda korokoroni kwa kufuata mkumbo?

Umeshawahi au kunusurika kwenda korokoroni kwa kufuata mkumbo?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Hii inaweza kumtokea mtu yoyote haijalishi unahusika Moja kwa Moja au lah!

Mimi nakumbuka Kuna siku rafiki yangu akuja na mteja anauza dsk 1tb kwa 20 tu basi kwasababu nilimwambiaga nahitaji hivo akaamua kumleta muuzaji kwangu

Basi sijui nn kilitokea Ila nikajikuta nimekataa kununua ile zaga basi akaniomba nimuazime hiyo 20 yeye ailipie halafu mimi nibaki na hiyo disk

Nikampa hiyo Hela akaniambia akileta Hela nitampatia dsk yake tukakubaliana ataniletea baada ya siku mbili

Sasa kesho yake ikaja gari sehemu ninapofanyia kazi akashuka askari na rafiki yangu na huyo muuzaji wa disk askari akaniambia

Wewe kijana ndo unatunza mali za wizi sio hebu kalete hicho kitu haraka Sana

Nikakimbia ndani chapu nikawaletea wakachukua na wale jamaa wakarudi ndani ya gari wakaondoka

Nafikiri pona yangu ni ile gari ilikuwa imejaa ni zile Kama tax maana yule dogo alikabidhiwa studio hivo alichukua vitu na kuanza kuuza mtaani aliwauzia wengi Sana

Jamaa walienda kukaa siku 3 hivi ndani na mpaka kutoka kibunda kiliwatoka.
 
Back
Top Bottom