Umeshawahi kuiba???

Daaaah nilikua naiba paper au marking scheme za paper kupitia dirishani kwenye ofisi za maticha alafu naenda kuwauzia majibu watoto wa kishua, ilikua nawapa majibu alafu wao wananipa hela au wananinunulia maandazi......actually mwisho wa siku nilishikwa baada ya kuchomeshwa na maboya flani flani...Ila since then nikawa goodboy
 
Hakuna hata mmoja anayeeleza kua bado anaiba,kila mtu kastaafu!!!!???
 
Sikawahi iba kiukweli
Ooooo ......! nimekumbuka niliwahi kuiba matikiti na kwenye shamba la jirani tukiwa shambani tunalima kufika saa 8 mzee njaa inauma Mama kakomaa mpaka tumalize kipande kilichobaki ndo turudi basi nikatoka kuzuga kama naingia kichakani kujisaidia mala nikaona matikiti kwenye shamba la jirani nikazama nikachuma nikalipasua chini kwa kulibwaga pwaa nikala then nikarudi kushika jembe tumbo liko safi kabisa
Wizi wa hela kwakweli hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…