Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Binafsi niliwahi kusinzia kwenye usafiri wa daladala hadi kupitilza kituo nilichokusudia kushuka. So, sikuona kama ni jambo la kushangaza sana.
Lakini leo hii Anti yangu ananisimulia kwa kushangaa alichokishuhudia kwenye daladala huko Dar es salaam, ati ameketi kwenye siti na pembeni yake kuna abiria mwingine aliesinzia na anakoroma na kuvibrate kama kiswaswadu, huku akistukastuka na kumuegemea mabegani mwake huku akiwa ameachama mdomo wazi kukoroma na udenda ukichuruzika...
Vipi wewe umeshakumbana na hali kama hii, kwenye dalalala mjini achilia mbali mabasi au safari ndefu za mikoani ambazo mara nyingi kuuchapa usingizi ni kawaida?