Umeshawahi kukutana na Walaghai wa Mitandao?

Umeshawahi kukutana na Walaghai wa Mitandao?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Walaghai wa Mitandao ni watu wanaofanya uhalifu wa mtandaoni kwa kuwasiliana na mlengwa kupitia barua pepe, simu, au ujumbe wa maandishi (SMS), wakijifanya wanatoka taasisi halali.

Lengo lao ni kuwarubuni watu kutoa taarifa nyeti kama vile taarifa binafsi, maelezo ya benki na kadi za mkopo, na nywila.

Taarifa hizo hutumika kuhamisha pesa au kufanya utapeli mtandaoni

Fahamu Jinsi ya Kutambua Walaghai hao wa Mitandao:

1. Hutumia ahadi kubwa za pesa au zawadi za thamani kubwa kuvutia watu.

2. Huwa wanasisitiza uchukue hatua haraka, kama vile kufanya malipo haraka au kukutaarifu kuwa nafasi ni za muda mfupi tu.

3. Usifungue kiambatanisho kutoka kwenye barua pepe ya mtu usiyemfahamu.

4. Usifungue ujumbe wala kubonyeza "link" kutoka kwa mtu usiyemfahamu.

NB: Epuka Kufuata maelekezo ya Walaghai wa Mitandao.
 
Mimi ninaye mmoja hapa kwenye whatsup ananiambia amenitumia I phone na laptop from usa to kenya airport through britishairways sasa mzigo ulipofika kenya kuna jamaa ananiambia nimtumie 65000tsh ili autume dar airport nilipo!
 
Natamani hata serikali ifatilie kuhusu hilo.....
Nilipigiwa simu asubuhi ya saa 4 nikaitwa kwa jina langu vizuri na nikajua ananifahamu, kwa kuwa namba ilikuwa ngeni nikauliza nani mwenzangu, akaniambia namba zangu ulifuta nikamwambia hapana nimebadilisha simu tu hivi karibuni nikumbushe wewe nani, akajitambulisha kwa jina la Imma tumesoma wote chuo na alikuwa akienda kwa jina la bahati pia, kwa kuwa nimemaliza chuo 2017 ni ngumu kuwakumbuka wote, me nikamueleza nimekusahau ila nieleze shida yako, akaniambia anafanya kazi kwenye maswala ya migodi, nikampa hongera akaniambia kunamchongo, akaniuliza kama ninakazi nikamwambia mimi nipo home tu, sina muelekeo wowote, akanza kunipa dili la hela kubwa linalofika milioni 9 na katika maelezo zangu milioni 3 😂, nilipoona mbona kiasi cha pesa ni kikubwa nikampigia miongoni mwa rafiki zangu niliosoma nao akaniambia kulikuwa hakuna mtu aliyeitwa jina hilo na alikuwa rafiki yangu, hapo na mimi nikajua hawa ni matapeli, nikasitisha mawasiliano nao papohapo
La kunishangaza ni kwamba namba yangu nimesajiliwa na mtu mwingine sio kwa jina langu ila aliniita kwa jina langu ninalotumia kabisa.
Sijaelewa hii imekaa vipi wana jamii!
TUjihadhari na utapeli wako makini sana katika mitandao yao
 
Back
Top Bottom