Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu, salama huko mlipoamkia?
Naamini wengi wetu tumekuwa tukipokea matangazo kwenye simu zetu ya huduma ambazo hatujawi kuzitaka, na hujawahi kutoa namba yako na kuwaruhusu kukutumia matangazo hayo.
Tena wakati mwingine wanataja mpaka jina lako, mf. Habari Cute Wife, unajua unaweza kujishindia milioni 10 ukitabiri mechi moja tu kwa usahihi? Sasa unabaki kushangaa eeeeh, yaani wana mpaka jina langu?
Unakuta upo ka mimi hujui hata kubeti lakini simu yako imejaa matangazo ya kubeti!
Kama hujatoa mawasiliano na kukubali kutumiwa matangazo haya ina maana namba yako imechukuliwa kimagendo kutoka sehemu fulani ambako uliwahi kuacha namba hii, mfano ulienda kwenye ofisi fulani ukatakiwa uandike jina na namba ya simu ili uweze kuingia, na wakati mwingine inaweza kuwa ni kutoka mtandao wako wa simu unaotumia, yale yaliyomfika Lissu ikawa ni extreme case sababu ya taarifa zako kuuzwa na kutumiwa vibaya.
Sasa umepatwa na kadhia hizi unajua wapi unatakiwa kwenda kushtaki na kulipwa maokoto yako kwa wizi huo wa taarifa zako binafsi?
====
Je, unatakiwa kuripoti wapi? Angalia maelekezo hapa👇👇

Endapo umepokea jumbe za namna hiyo bila ridhaa yako au bila kumpatia mtuma ujumbe namba zako unatakiwa kuwasilisha malalamiko hayo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo imeanzishwa kwa lengo la kusimamia na kulinda Taarifa Binafsi na faragha za watu nchini.
Malalamiko hayao yanaweza kuwasilishwa njia ya kwa maandishi au unaweza kuwasiliana nao kwa njia ya simu ukapewa mwongozo zaidi.
Tume hiyo imeanzishwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022. Kwa msaada zaidi tembelea tovuti yao. Na kizuri ni kuwa hakuna presha ya kuwaza kuhusu pesa za wakili kusimamia madai yako, wadau wapo kusimamia sehemu hii kuhakikisha unapata haki yako na kila aliyehusika kwenye kuingilia faragha yako anawajibika ipasavyo
pye Chang shen Nyoka kibisa Kudasai TheChoji